Wilfred Lwakatare (kushoto) na wenzake wakifuatilia kesi yao mahakamani. |
Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam imeita majalada ya kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph kwa ajili ya kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliowafutia washitakiwa hao mashitaka ya ugaidi.
Hatua hiyo inatokana na maombi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kupinga uamuzi huo na kuiomba Mahakama iufanyie marejeo na kuamuru kuwa haukuwa sahihi kisheria.
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza alisema ameshapokea amri ya Mahakama ya Rufaa kuitisha jalada la kesi hiyo lililopo katika Mahakama hiyo pamoja na la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mei 8 mwaka huu, Jaji Lawrence Kaduri alifuta mashitaka matatu ya ugaidi dhidi ya washitakiwa hao kwa kuwa hati ya mashitaka iliyofunguliwa na DPP, haielezi uhalisia wa kosa hilo na washitakiwa wanahusika vipi kufanya ugaidi.
Katika ombi hilo, Mkurugenzi wa Mashitaka anaiomba Mahakama iite na kuangalia rekodi za Mahakama Kuu kwa nia ya kujiridhisha usahihi, uhalali wa uamuzi huo pamoja na amri zilizotolewa.
Aidha anaomba Mahakama kufuta uamuzi kuhusu uhalali wa mashitaka wanayodai yalikuwa ya awali, ione kuwa walalamikiwa walikuwa hawajaitwa kujibu mashitaka yao, pia haikuwa sahihi kwa Mahakama hiyo kuamua kuhusu uhalali huo.
Anaomba Mahakama ione kwenye sababu zilizoombwa na walalamikiwa katika ombi lao, hakuna ombi la kufuta mashitaka dhidi yao, pia hakuna taarifa zilizowasilishwa na walalamikiwa ambazo Mahakama Kuu ingeamua uhalali wa mashitaka au kuwepo kwa mapungufu.
DPP anaomba Mahakama iamuru kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu, kufuta baadhi ya mashitaka kwenye hati ya mashitaka ya muda haukuwa sahihi kisheria.
Lwakatare kwasasa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa na Mahakama kwa kuwa mashitaka yanayomkabili yana dhamana.
Washitakiwa hao wanadaiwa Desemba 28 mwaka jana katika eneo la King’ongo, Kinondoni, Dar es Salaam walipanga njama ya kutenda kosa la jinai la kutumia sumu kumdhuru Mhariri wa gazeti la Mwananchi Dennis Msacky
إرسال تعليق