"Kama
yeyote anayekuja wakati unamtii kiongozi, na kujaribu kuvuruga umoja
wao na kuwatawanya, muue," alinukuu hadithi ya Mtume Mohammad kama
ilivyopokelewa na Sahih Muslim.
Kamanda wa juu wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane alitumia maneno kama hayo kutishia idadi inayoongezeka ya waasi ndani ya kikundi hicho cha wanamgambo kupitia taarifa aliyotoa tarehe 17 Juni. Ilikuja siku mbili kabla ya wanamgambo watiifu kwa Godane kuingia katika mapambano ya kumwaga damu huko Barawe na wanachama wa al-Shabaab wa kikundi kilichojitenga wanaopinga utawala wake. Waasi wamepinga kile walichokieleza kama tabia yake iliyoongezeka kuwa ya kidhalimu.
Taarifa hiyo ya kurasa 17 iliyotolewa na kitengo cha habari

cha
al -Kataib cha kikundi hicho cha wanamgambo kupitia Twitter, yenye
kichwa cha habari "Hii ni Taarifa kwa Watu" ni ushahidi wa wazi wa
kuongezeka kwa shinikizo la ndani kuhusu Godane. Taarifa hiyo ilieleza
kwa kina ukiukaji dhahiri wa waasi, na majaribilo ya kutumia orodha
ndefu ya hadithi na aya za Kur'an kulazimisha utiifu ndani ya safu ya
askari wa al-Shabaab na kuhalalisha msako wa watu unaoendelea wa Godane.
"Kwa wale wanaofuatilia matukio ya Somalia, malalamiko yasiyo na ukweli na uongo uliochapishwa hivi karibuni kwenye tovuti na vyombo vya habari vya kijamii imekuwa dhahiri," taarifa ilisomeka. "Kashfa zenye karaha na uongo uliolenga mtazamo wa al-Shabaab, mpangilio, uongozi na askari, kama tuhuma zilizotolewa na baadhi ya mujahidina waliokubali na kutoa maoni mabaya wa umma wa Mohammed, amani iwe juu yake, na kuwa katika mikono ya maadui wa taifa ili kulisaliti."
Godane anarejelea idadi kubwa kulaaniwa dhahiri uongozi wake kutoka kwa viongozi waandamizi wa al-Shabaab na wapiganaji wa nje, ikiwa ni pamoja na al-Zubayr al-Muhajir hapo tarehe 20 Aprili na Ibrahim al-Afghani hapo tarehe 6 Aprili. Kiongozi wa ngazi ya juu wa al-Shabaab pia alilenga wafuasi wa Mujahidina mzaliwa wa Marekani Omar Hammami, ambaye pia anajulikana kama Abu Mansoor al-Amriki. Zaidi ya mwaka mmoja wa kumpinga dhahiri Godane kupitia mfululizo wa video na shughuli za Twitter zilisimama mapema Mei, baada ya vyombo vya habari vya ndani kuripoti wauaji wamuua kwa bunduki al-Amriki.
Kauli na tangazo lake katika mtandao wa Twitter linaonekana kwa Kiarabu tu. Kwa kuzingatia kwamba kauli hiyo inajaribu kuwekwa kwa ajili ya wasomaji wa kiarabu tu, na kwamba mada inayohusika ni utii kwa Godane, walengwa wanaweza kuwa wanamgambo wa kigeni nchini Somalia ambao uhusiano wao na yeye umetoweka pamoja na kuwapa vyeo maulamaa wa Kisomali ambao wanaweza kusaili kuhusu uongozi wake.
"Kauli hii imekuja baada ya ukimya wa miaka mingi, kwani tuna matumaini ya kupatana nao, tulikuwa na mawazo mazuri juu yao na kusuburi zamu yao katika kweli," tamko liliendelea. "Hata hivyo, walidumu katika udanganyifu, alisisitiza katika mwelekeo wao na kufuata matakwa yao."
Kusitisha kusambaa kwa mafarakano ndani ya safu pia ni moja ya hoja za waraka huo, kwani unaeleza kwamba "mujahidina hawapaswi kurudia kila kitu ambacho wanakisikia na wanapaswa kuacha kuteta na kuuliza maswali".
Kugeuza maneno ya Kur'an na ya Mtume Mohammad
"Anachokifanya Ahmed Godane, anaponukuu baadhi ya aya za Kur'an na hadithi bila ya muktadha au kuzinukuu ili kuunga mkono matukio kadhaa ambayo kimsingi hayakutolewa katika kujaribu kuhalalisha kuwatafuta na kuwaua wapinzani wake, inachukuliwa kama upotoshaji wa Uislamu," alisema Sheikh Ibrahim Abdullahi, mhubiri wa dhehebu ya Sunni kutoka Ahlu Sunna wal Jamaa.
"Godane sio kiongozi halali wala mlezi wa Waislamu, na madai yake ya utii uliozidi kiasi yanasimama katika upinzani kwa imani ya sharia za Kiislamu kwa sababu kadhaa," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Kwanza kabisa, sio kiongozi halali wa Waislamu, bali kiongozi wa kikundi cha uasi na utawala wake ni wa ukatili kuliko unaokubalika. Pili, anaamuru vitendo vyenye dhambi kama vile umwagaji damu wa raia wasio na hatia na anatumia mkabala wa takfiri kwa kuwaona viongozi wa serikali kama waovu bila ya kubagua."
"Al-Shabaab inajulikana kwa kutafsiri vibaya na kutumia vibaya Uislamu ili kuwapotosha watu wasiyo na elimu na wapiganaji vijana ambao hawauelewi vizuri," Abdullahi alisema. "Hii ni sehemu ya mkakati unaotumiwa mara kwa mara na viongozi wa al-Shabaab kuwafanya watu wasioamini kuzingatia tafsiri mbaya ya Uislamu."
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Mogadishu Hussein Nur Guled alikubaliana na hayo.
"Al-Shabaab inatumia ufafanuzi huo huo wa Uislamu wenye makosa ambao unawaruhusu kumwaga damu ya Wasomali wasio na hatia hadi sasa kuuwana wao wenyewe," Guled aliiambia Sabahi. "Kama usemi wa kale unavyosema 'wawili wanaokula njama za kutotenda haki watapambana dhidi ya haki' na hiyo ndiyo hali ya al-Shabaab leo hii, kwa sababu wanapigania jambo linalofanana [utawala usio wa haki] waliouanzisha wenyewe."
"Sasa inaeleweka wazi kwa watu wa Somalia kwamba al-Shabaab hawahusiki kabisa na dini, bali walikuwa wanaitumia kufanikisha matakwa yao ya kisiasa," alisema. "Walishindwa katika hilo kwa sababu sasa wamegawanyika katika vikundi kwa kila kimoja kujichukulia uhalali kwao kumwaga damu ya wengine kwa kutafsiri vibaya Kur'ani na hadithi za Mtume kwa matakwa yao."
Mtume Mohammad na utii wa sheria
Utii wa anayetwala, kama ilivyoagizwa na Mungu na Mtume Mohammad, hauwezi kuwa wa upofu na kabisa, alisema Sheikh Abdullahi.
"Utii kwa kiongozi ni katika mazingira ambayo hakuna dhambi au kufanya matendo mabaya, na hili ni jambo ambalo limekuwa likihubiriwa kwa kuzingatia kile alichokisema Mtume Mohammad, amani iwe juu yake," aliiambia Sabahi.
Abdullahi alinukuu hadithi tatu husika ya Mtume Mohammad:
• "Mwislamu anapaswa kuwa mtii iwapo ni kwa kitu wanachokipendelea au wanachokichukia isipokuwa kama ni kitendo cha dhambi. Kama wataagizwa kufanya dhambi, hawapaswi kusikiliza au kutii" -- kama ilivyopokolewa na Bukhari na Muslim.
• "Hakuna utii kwa kilichoumbwa kama inamaanisha kutomtii Muumba" – kama ilivyopokolewa na Ahmed na Hakim
• "Hakuna utii kwa mtu fulani kama inamaanisha kutomtii Mungu. Utii ni kwa fadhila tu" -- kama ilivyopokolewa na Bukhari na Muslim
Sheikh Omar Abdirahman, mjumbe wa chama cha Wanazuoni wa Kiislamu wa Somalia, aliiambia Sabahi kwamba msimamo wa Godane wa kuwapa majina viongozi wengine wapinzani wa al-Shabaab kama makafiri au wanafiki unapingana na sheria za Kiislamu.
"Kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Godane anawapa jina la kafiri au kuwatisha au kuwaua wale wanaopinga mawazo yake," alisema Abdirahman.
"Godane sio kiongozi aliyechaguliwa ambaye anapaswa kutiiwa, na kwa sababu alitoa tamko ni kufanya liwe halali kisheria kwa yeye kuwaua wale wanaompinga," alisema.
"Hii ni kinyume na kanuni za Kiislamu, lakini anatumia jina zuri la dini kutimiza dhamira yake," alisema Abdirahman.

إرسال تعليق