Na Elias Msuya (email the author)
Kwa ufupi
- Uchunguzi uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ulithibitisha kwamba, Kamanda Kamuhanda, alisimamia moja kwa moja mauaji ya mwanahabari huyo, kwani kabla ya kuuawa kwake alikuwa mikononi mwa polisi chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Kamuhanda
Taarifa za kupandishwa cheo kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, haziwezi kupita bila kujadiliwa.
Mbali na maofisa wengine wa jeshi hilo waliopandishwa vyeo, Kamuhanda amepandishwa cheo kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi ( DCP).
Kamuhanda ambaye kabla ya Iringa alikuwa kamanda wa polisi mkoani Ruvuma, na alihamishwa baada ya tukio la askari kuwaua kwa risasi waandamanaji ambao ni madereva wa bodaboda.
Akiwa mkoani Iringa nako mkosi wa mauaji ukaendelea, kwani mwaka 2012 alikumbwa na tuhuma za kuamrisha mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel 10, marehemu Daudi Mwangosi.
Uchunguzi uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ulithibitisha kwamba, Kamanda Kamuhanda, alisimamia moja kwa moja mauaji ya mwanahabari huyo, kwani kabla ya kuuawa kwake alikuwa mikononi mwa polisi chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Kamuhanda.
Hata hivyo, Serikali nayo iliunda timu yake ya uchunguzi ambayo ripoti yake imefichwa kwa kisingizio cha kesi kuwa mahakamani.
Kisingizio hicho ndiyo kimekuwa kikitumika kumlinda Kamanda Kamuhanda kuendelea na wadhifa wake tena katika mkoa huo huo, na sasa amepandishwa cheo.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani kupitisha bajeti yake, huku Waziri wake Dk Emmanuel Nchimbi akiwaambia wabunge kuwa suala hilo halipelekwi kisiasa, ndiyo maana Kamuhanda ameendela na cheo chake.
Kama hiyo haitoshi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenela Mukangara hakugusia chochote kuhusu mfululizo wa mateso ya waandishi wa habari katika hotuba ya bajeti yake.
Hiyo ni kumaanisha kuwa Serikali haina mpango wowote wa kulinda maisha ya raia wake, bali kulinda maslahi ya viongozi wachache.
Sikatai, inawezekana kisheria, Kamuhanda akawa na haki na wala sipingi kupandishwa kwake cheo tu, lakini kwa kuzingatia maadili na utu haiwezekani mauaji yatokee mikononi mwa kiongozi, halafu apandishwe cheo. Huo siyo utamaduni wa Mtanzania, ni kebehi tu ya viongozi wetu.
Kebehi hii haikuanza leo, kuna mifano mingi tu. Hata mwaka 2000 baada ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuuawa baada ya kufanya maandamano, Rais Benjamin Mkapa aliwapandisha vyeo maofisa wa polisi waliosimamia operesheni
.Chanzo:- mwananchi

إرسال تعليق