MUANGAZA KUTOKANA NA NURU YA UTUME
Imepokewa kwa Usama Ibn Zaid amesema: nilisema ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu sijakuona ukifunga katika mwezi wowote hivi unavyofunga katika
mwezi wa Shaabani? Akasema Mtume huo ni mwezi ambao watu wanaghafilika
nao baina ya Rajab na Ramadhan na huo ni mwezi ambao amali za watu
hurufaishwa kwa bwana wa viumbe kwa hivyo nnapenda zirufaishwe amali
zangu na hali mimi ni mwenye kufunga”
Sahihi Targhiib (1022)
Bismillahir Rahmanir Raheem
Hakika saumu ni ibada kubwa na ni siri baina ya mja na Mola wake wala
haijui siri hiyo isiyo yeye na waja huwa wakaijua siri hiyo kwa kuacha
vitu vyenye kufunguza vya dhahir, ama kuwa mtu amewacha chakula chake na
kinywaji chake na matamanio yake kwa ajili ya Mola wake hilo ni jambo
ambalo hawawezi kulijua watu na hiyo ndiyo hakika ya saumu.(1)
Post a Comment