Mke wa Rais na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete
akimkaribisha kwa mazungumzo Profesa Midori Uno, anayefundisha somo la
kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Soka kilichoko huko Tokyo nchini Japan.
Mama Salma alikutana na mgeni wake huyo kwenye hoteli ya
Intercontinental huko Yokohama leo. PICHA NA JOHN LUKUWI.
Na Anna Nkinda – Yokohama
Watumiaji
wa lugha ya Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia
hatua ya kuwa na mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka
kilichopo nchini humo.
Hayo
yamesemwa leo na Prof. wa chuo hicho Midori Uno wakati akiongea na Mke
wa Rais mama Salma Kikwete alipokutana naye katika hoteli ya
Intercontinental mjini Yokohama.
Prof. Uno ambaye ni Mwalimu wa kiswahili katika chuo hicho alisema
kuwa hivi Sasa wananchi wengi wa Japani wanakiu ya kujifunza na
kuzungumza lugha ya Kiswahili kwani ni rahisi kueleweka.
“Katika jitihada zangu za
kuwafanya wajapani wengi wajue lugha ya Kiswahili nimetengeneza kamusi
ya maneno ya kijapani kuwa ya Kiswahili ambayo watu wengi wanaitumia
kwa sasa kwani wengi wajapani wengi wanapenda kujifunza lugha hii”,
alisema Prof. Uno.
Mashindano hayo ya lugha ya Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila mwaka huwa ni ya kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa cheti, tuzo ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake Mke wa Rais mama Kikwete alimpongeza profesa huyo kwa jitihada zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini humo na kumuomba aendelee zaidi kufanya hivyo.
Mashindano hayo ya lugha ya Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila mwaka huwa ni ya kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa cheti, tuzo ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake Mke wa Rais mama Kikwete alimpongeza profesa huyo kwa jitihada zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini humo na kumuomba aendelee zaidi kufanya hivyo.
Alisema
kuwa watanzania wanavitu vyao vya kujivunia kama Taifa, moja ya vitu
hivyo ni lugha ya Kiswahili ambayo imewaunganisha watanzania wote na
kuwa kitu kimoja ndani na n je ya nchi.
Mama
Kikwete alisema, “Ili kumfikia mtu mmoja au watu wengi zaidi ni lazima
kuwe na lugha ya mawasiliano hivyo basi nasi tunatumia lugha hii
ambayo iliwaunganisha watanzania wote wakaweza kupigania uhuru wa n chi
yao kipindi cha mkoloni”.
Alisema
kuwa lugha ya Kiswahili inaongelewa maeneo mengi ya Afrika ya mashariki
na ndani ya bara la Afrika na hivi sasa viongozi wa Umoja wa Nchi za
Afrika (AU) waliikubali lugha hiyo kuwa lugha ya mawasiliano .
Profesa Uno alikuja nchini kabla ya kupata uhuru kwa ajili ya kufanya
kazi za kujitolea na aliporudi nchini kwake aliamua kuwafundisha
wajapani lugha ya Kiswahili pia nchini humo redio Japani (NHK)
inatangaza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilianzishwa
mwaka 1964
Post a Comment