Na Mwandishi Wetu
MBIVU na mbichi sasa zinaweza kujulikana, kinachoombwa ni muda tu, kwani mng’amuzi halisi kuhusu kifo tata cha mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa Bongo, Albert Mangwea ‘Ngwea’, yupo kwenye mazingira mazuri kueleza kilichotokea.
KWA NINI ANA USHAHIDI WOTE?
Mwanamuziki
wa Bongo Fleva, Mgaza Pembe ‘M2 The P’, ndiye mwenye ushahidi wote
kwani aliambatana na Ngwea kila sehemu waliyotembelea mpaka nukta ya
mwisho nchini Afrika Kusini.
M2
The P, alipatwa na matatizo sawa na marehemu Ngwea, isipokuwa mwenzake
ilifikia hatua mbaya na kupoteza maisha huku yeye akibaki mahututi
kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika
Hospitali ya St. Helen Joseph, jijini Johannesburg nchini humo.
Jambo
la faraja ni kwamba, M2 The P yupo vizuri kwa sasa, atakaporuhusiwa
kutoka, atajibu maswali mengi tata ambayo yamejitokeza tangu Ngwea
alipofariki dunia Juni 28, mwaka huu, nchini humo alipokwenda kwenye
shughuli zake.
JAWABU LA SUMU
Moja
ya mambo yanayozungumzwa pembeni ni kwamba kuna uwezekano mkubwa
marehemu Ngwea na M2 The P waliwekewa sumu kwenye chakula au
kupuliziwa ‘laivu’ kisha kutokea yaliyotokea, lengo likiwa kuwadhulumu
mzigo wa fedha nyingi waliokuwa nao, hivyo kupona kwa mmoja huyo ni
matakwa ya Mungu ili awe shahidi namba moja wa kifo cha Ngwea.
“Ni
jambo la kumshukuru Mungu jamani, M2 The P anaendelea vizuri sana, kwa
sasa anazungumza. Naamini yeye amepona kwa ajili ya kufichua
kilichofichika nyuma ya kifo cha mwenzake.
“Kama
kweli walilishwa sumu kwenye chakula au walipuliziwa au lolote lile
lingine, M2 The P anajua kila kitu kwani walikuwa wote kwa siku nzima
mpaka wanarudi nyumbani alfajiri kwa safari ya kurudi Bongo.
“Awali
tuliposikia M2 The P naye amefariki dunia sisi Wabongo wa huku
tuliumia sana, tukasema sasa nani atafichua kilichotokea? Lakini Mungu
mkubwa,” alisema Tony, Mbongo anayeishi Sauzi akifanya biashara halali.
HOFU YA KUUAWA M2 THE P.
Baadhi
ya watu waliishauri Serikali ya Tanzania kufanya kila liwezekanalo, M2
The P alirudi Bongo wakidai kama kweli wawili hao walilishwa sumu kwa
namna yoyote ile, wahusika watafanya juu chini kuuondoa uhai wake ili
kupoteza ushahidi.
Walisema kama ni sumu, wahusika watakuwa bado wapo
ndani ya nchi hiyo na kwa vile M2 The P hana ndugu wa damu kule, si
rahisi kulindwa kwa kiwango cha kutambua nani mbaya kwake.
MADAI YA UNGA KWA M2 THE P
Kumekuwa
na madai kwamba, Ngwea alifariki dunia kwa ‘kujiovadozi unga’ lakini
kama kweli msanii huyo alikuwa akitumia ‘mambo’, madai hayo yanapingana
na ukweli kuhusu M2 The P kwamba si mtumiaji wa unga.
Kwa
maana hiyo kama M2 The P si mtumia unga kwa nini na yeye alikumbwa na
dhahama ileile iliyomkumba mwenzake? Kuna zaidi ya kitu hapo.
Juzi,
Uwazi liliwatafuta baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva waliowahi kufanya
kazi karibu na M2 The P na kuwauliza kama wanajua chochote kuhusu madai
ya msanii huyo kubwia unga kama Ngwea, wote walikanusha.
“Jamaa
(M2 The P) hatumii unga, we si unaona hata afya yake? Mtu anayetumia
unga anajulikana hata kwa macho kaka,” alisema Mbongo Fleva mmoja
mwenye jina kubwa Bongo akitokea upande wa Temeke.
Ndugu mmoja wa
karibu na msanii huyo alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai hayo,
alisema aliwahi kusikia tetesi hizo mwaka jana, alipofanya uchunguzi
alishindwa kupata ukweli huku mtuhumiwa mwenyewe akikataa katakata
kubwia madawa ya kulevya.
DALILI ZA MBWIA UNGA
Kwa mujibu wa kitaalam, binadamu anayetumia unga hupoteza nguvu na uwezo wa kufanya mambo aliyokuwa akimudu kuyafanya awali.
Akizungumza
na Uwazi juzi, daktari wa zahanati moja iliyopo Kimara, Dar es Salaam
(jina tunalo) alitoa mfano wa kitaalam kwamba, mcheza mpira anayemudu
kukaa uwanjani kwa dakika 90 anapotumbukia kwenye matumizi ya madawa ya
kulevya hupoteza uwezo huo na pengine kumudu kuwepo kwa dakika 45 tu.
Alisema
unga una tabia ya kummaliza nguvu mtumiaji, hasa asiye na uwezo wa
kupata lishe nzuri hivyo kupoteza uwezo mkubwa wa awali, jambo
linaloweza kuwafanya wengine kuona mabadiliko hayo ya wazi.
“Kuna
mchezaji wa timu moja kubwa nchini, awali alikuwa akisifika kwa kucheza
mpira vizuri, tena kwa muda wote, alipoanza kutumia unga uwezo wake
uwanjani ulishuka kabisa na ikafika hatua akawa hapangwi hadi kiongozi
mmoja wa timu alipombaini,” alisema dokta huyo.
M2 THE P ALICHEZA MPIRA KWA DAKIKA 90
Julai
7, 2012 kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini linalofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar kila mwaka (hata mwaka huu lipo), M2 The P alichezea Timu ya
Bongo Fleva inayowashirikisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Msanii
huyo alimudu kucheza mpira kwa dakika zote 90, hali inayoweza kuondoa
wasiwasi kwamba ni mtumiaji wa unga kama inavyodaiwa.
إرسال تعليق