Naibu waziri wa mambo ya nje wa Qatari Ali bin Fahd al-Hajri na Jan Mohammad Madani, mmoja wa maafisa wa Taliban akikata utepe katika ufunguzi rasmi wa ofisi y aTaliban huko Doha, Qatar, June 18, 2013.Marekani imetangaza kwamba itaanza majadiliano na kundi la Taliban baadaye wiki hii katika juhudi za kubuni mpango wa kumaliza zaidi ya muongo mmoja wa vita nchini Afghanistan.
Maafisa wa Marekani wanasema mazungumzo yataanza Alhamisi mjini Doha, mji mkuu wa Qatar. Maafisa wa yeo vya juu wa wizara ya mambo ya nchi za nje na White House wanatazamiwa kukutana na ujumbe wa Taliban katika kile kinachoelezwa ni mazungumzo ya awali.
Maelezo ya mazungumzo hayo yalitolewa wakati maafisa wa ulinzi wa Marekani kuthibitisha kwamba wanajeshi wanne wa Marekani waliuliwa jumanne katika kambi ya jeshi la anga kwenye uwanja wa ndege wa Bagram Kaskazini mwa Kabul. Maafisa walihusisha vifo hivyo na shambulio la waasi la mzinga na roketi , lakini hawakutoa maelezo zaidi.
Akizungumza kwenye mkutano wa mataifa tajiri G8 huko Ireland ya kaskazini rais Barack Obama aliyaeleza mazungumzo ya Qatar kuwa ni hatua ya kwanza kabisa na kutahadharisha kwamba anatarajia kutakuwa na vizingiti vingi vitakavyohitaji kuondolewa.
Serikali ya rais Hamid Karzai wa Afghanistan hatarajiwi kushiriki katika duru ya awali ya mazungumzo ya Doha. Lakini maafisa wanasema mazungumzo yanatarajiwa kupelekea kuwepo na mkutano kati ya Taliban na baraza la amani lililoungwa na wazee na viongozi wa Afghanistan.
Hadi hii leo Taliban wamekataa kuzungumza hadharani na serikali ya Karzai. Rais Karzai alisema jumanne kwamba serikali yake itapeleka wajumbe Qatar kujaribu kuanzisha mazungumzo ya amani Kabul na Taliban.
- Dw
إرسال تعليق