Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma
Kikwete akipokea ua kutoka kwa msichana anayetunzwa katika kituo cha
watoto wa kike watukutu cha Pertapis kilichoko Singapore wakati
alipokitembelea kituo hicho tarehe 6.6.2013. Mama Salma yupo nchini
Singapore akiambatana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku
mbili nchini humo. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Mama Sahnim Sokaimi.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu
wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis
kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na uongozi wa
kituo cha kuwatunza wasichana na wanawake watukutu cha Pertapis
kilichoko nchini Singapore.
Mwenyekiti
wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa
kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha kuwarekebisha tabia
wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko Singapore wakati
alipokitembelea tarehe 6.6.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mama Badriya
Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA,
Mama Salma Kikwete akizungumza na Mama Sahnim Sokaimi, Mkuu wa kituo cha
kurekebisha tabia za wanawake na wasichana watukutu cha Pertapis
kilichoko nchini Singapore mara baada ya kukitembelea tarehe 6.6.2013.
إرسال تعليق