Mshindi wa Fastjet: Nitakwenda Zanzibar na mchumba wangu

Msanii wa filamu nchini Ndeshi Wakwe ambaye amekuwa abiria wa laki mbili kukata tiketi ya kusafiri wa shirika la ndege la Fastjet na kujishindia safari ya siku mbili katika Hotel ya Serena ya Zanzibar amesema atatumia safari hiyo kwenda na mchumba wake.

Ndeshi ambaye ameonekana mara kadhaa katika matangazo mengi ya biashara na tamthilia ya Awaking ambayo inaonyeshwa na kituo cha Africa Magic akiwa sambamba na waigizaji wengine kama Mzee Chilo, Baby Madaha, Muhogo Mchungu, Mama Mjata na Mama Mpangala hakutaka kuanika jina la mchumba wake.

“Fastjet wameni-surprise sana maana hii ni mara yangu ya kwanza kusafiri nao na sasa watawezesha mie kwenda Zanzibar ambako sijawahi kufika toka nizaliwe, so nimefurahi sana” anasema Ndeshi

Ndeshi ameshinda safari hiyo baada ya kuwa abiria wa lakini mbili kukata tiketi ya kwenda Kilimanjaro. Akiongea kwa njia ya simu na tabianchi amesema “Nitazungumza na mchumba wangu juu ya safari hiyo ili kuona kama atakuwa na nafasi ya kujumuika nami”.


Fatjet imekuwa ikitoa zawadi kwa abiria wake ikiwa ni moja ya njia ya kurejesha shukrani zake kwa wateja wake.

Post a Comment

أحدث أقدم