Lt.
Jenerali Paul Ignace Mella,Mkuu Mpya wa Jeshi la Mseto kati ya Umoja wa
Mataifa na Umoja wa Afrika maarufu kama UNAMID linalolinda Amani huko
DARFUR Nchini Sudan.
Lt.
Jenerali. Mella kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) anachukua
nafasi iliyoachwa na Lt. Jenerali Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye
amemaliza muda wake Machi 31,2013.
---------
Kwa mara nyingine Bendera ya Tanzania imeendelea kupepea katika Tasnia ya Ulinzi wa Amani ya Kimataifa.
Mapema
wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika Bi. Nkosizana Dlamin Zuma wametangaza...
uteuzi wa Luteni General Paul Ignace Mella Kutoka Jeshi la Wananchi wa
Tanzania ( JWTZ) kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa
Mataifa huko Darfur ( UNAMID)
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, na
nakala yake kutumwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, imeeleza kwamba, Lt. Gen. Mella
anachukua nafasi iliyoachwa na Mkuu wa zamani wa Jeshi hilo (UNAMID),
Lt. Gen Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye amemaliza muda wake wa
utumishi March 31,2013.
Wasifu
wa Luteni General Paul Ignace Mella unaelezwa kuwa ni Mwanajeshi wa
muda mrefu na mwenye uzoefu na utumishi uliotukuka katika JWTZ akiwa
amewahi kushika nyadhifa mbali mbali muhimu za uongozi.
Baadhi
ya nyadhifa hizo ni pamoja na Naibu Kamanda Kikosi cha Tanzania chini
ya Umoja wa Mataifa huko Liberia ( 1993-95), Kamanda wa Kikosi cha JWTZ,
Afisa Mnadhimu-Makao Makuu ya Jeshi, Mwambata Jeshi-Ubalozi wa Tanzania
Uganda na hadi sasa alikuwa ni Mkuu wa Usalama na Utambuzi- JWTZ.
Uteuzi
wa Lt. Generali Mella unafuatia mchakato mrefu ulioshindanisha
wateuliwa kutoka nchi mbalimbali duniani, na hatimaye yeyé akaibuka
mshindi.
Post a Comment