Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika moja ya kikutno mkoani Njombe.
Na Mwandishi Wetu Makambako
Na Mwandishi Wetu Makambako
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeibua
mipango ya siri ya mauji inayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), kwa kuwahusisha askari Polisi na wananchi wa kawaida.
Hatua hiyo ya CCM kuvunja ukimya kuhusu
sakata hilo
liliibuliwa jana mjini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi
Taifa, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa Makambako na
vitingoji vyake.
Katika mkutano huo Nape, alisema kuwa
kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA ya kufanya maandamano ambayo
yataambatana na mauji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo.
Alisema mipango hiyo imekuwa ikiratibiwa
kwa mwezi mmoja sasa kwa kufanyika vikao katika maeneo tofauti kwa kuwahusisha
viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho cha upinzani.
“Ninapenda kuweka wazi jambo moja kwa
mujibu wa taarifa za siri ambazo CCM imezinasa kutoka ndani ya CHADEMA ni
kwamba hivi sasa chama hiki kipo katika mikakati ya kufanya maandamano katika
miji minne ikiwemo Makambako.
“Lengo la maandamano hayo ni kuibua
vurugu zitakazosababisha mauji dhidi ya askari Polisi na raia wa kawaida ili kutafuta
umaarufu wao ambao umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni.
“CCM inapenda kuwaambia Watanzania
popote pale walipo wajue kuwa CHADEMA si chama cha siasa, bali ni genge la watu
ambalo limejikusanya kwa lengo la kuua na kung’oa kucha watu. CCM haiko tayari
kuona nchi inaingia katika shimo la mauji ya kupanga hata kidogo.
“Kwa wiki moja sasa wamekuwa wakichagua
miji ya kufanya maandamano yao
ambayo yataambana na mauaji na wamepanga kufanya katika miji ya Makambako,
Songea pamoja na miji ya Ilula wilayani Kilolo pamoja na mji wa Ruaha wilayani
Kilombero,” alisema Nape huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano
huo.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Taifa, alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kimya na kuacha vyombo vya
dola vifanye kazi yake hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitaka kulitumbukiza
taifa katika machafuko kwa kivuli cha siasa.
Alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa
CCM haitakuwa tayari kuona mauji kutokea tena nchini kama
ilivyokuwa katika miji ya Arusha, Morogoro na Iringa.
“Ni wazi siku tatu kabla ya maandamano
ya Morogoro yaliyosababishwa kifo cha kijana mmachinga asiye na hatia, CCM
ilijitokeza mbele ya umma wa Watanzania na kuwaambia kuwa kuna mipango ya
mauaji inayopangwa na CHADEMA kwa kutoa watu jijini Dar es Salaam.
“Ilipotimu siku hiyo walifanya hivyo kwa
kutoa magari kila kona ya jiji la Dar es Salaam na kwenda kuwaingia vijana
maskini wa Morogoro katika maandamano ambayo yalipigwa marufuku na Polisi.
“Haikupita muda alikufa kijana wa
kitanzania bila hatia huku Mbowe na babu Slaa wakiwa Dar es Salaam wakiendelea na kazi zao huku
wakifanya mashauri na familia zao. Kama wao
kweli wana uchungu na nchi hii kwani hatuwaoni wakiwa mbele ya maandamano,”
alisema Nape.
Kutokana na kauli hiyo Nape, alisema
kuwa moja ya kazi anayoifanya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, ni kwenda
mjini Songea ambapo atafanya kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.
Emmanuel Nchimbi na kumueleza mipango hiyo michafu inayolenga kuharibu sifa ya Tanzania.
Mwisho
إرسال تعليق