WATU WATANO WAFARIKI DUNIA BAADA YA MALORI MATATU KUPATA AJALI MASEYU MOROGORO.

WATU watano wamefariki dunia baada ya kutokea kwa ajali ilihusisha magari matatu katika eneo la Maseyu tarafa ya Mikese katika barab
ara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro katika tukio lililotokea majira ya saa 1:45 usiku wa Juni Mosi mkoani hapa. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

 

Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao akizungumza katika eneo la tukio alisema kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu aina ya Mistubishi Fuso lenye namba ya usajili T 855 BZW kugongana na Scania zenye namba ya usajili T 657 AFJ yaliyogongana uso kwa uso na wakati yakitaka kulipita scania nyingine yenye namba ya usajili na T 827 AJJ ambayo ilishindwa kupanda mlima na kuziba robotatu ya barabara na kupelekea watu watano kufariki dunia na majeruhi wawili.

Post a Comment

أحدث أقدم