Shirika la
upelelezi la Marekani FBI limesema kuwa barua yenye sumu hatari aina ya
ricing imetumwa kwa rais Barack Obama kutoka Spokane katika jimbo la
Washington, siku ambayo barua ya sumu kama hiyo ilipotumwa kwa Jaji wa
mahakama kuu na kwa posta.
Mtu mmoja
alikamatwa wiki iliyopita huko Spokane kuhusiana na barua hiyo
iliyotumwa kwa jaji na ambayo ilizuiliwa tarehe 14 mwezi huu.
FBI imesema
barua iliyokuwa imetumwa kwa rais Obama iligunduliwa tarehe 22 na
kuongeza kuwa barua nyingine kama hiyo ilikuwa imetumwa kwenye kituo cha
ndege za kijeshi kilicho karibu.
Taarifa ya FBI na ya huduma za posta imesema kuwa barua zote 4 ziliwekewa stampu tarehe 13 Mei huko Spokane.
Tatu kati ya barua hizo zimethibitishwa kuwa na sumu ya ricin na nyingine moja bado inachunguzwa.
SOURCE-DW
إرسال تعليق