Obama kukutana na familia ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela

Barack Obama and Jacob Zuma hold a joint news conference in Pretoria today. The U.S. President said the thoughts of Americans and people around the world were with Nelson Mandela and his family
Kushoto ni Rais wa Marekani Barack Obama, kulia ni mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
REUTERS/dailymail


Rais wa Marekani Barack Obama atakutana na familia ya mwasisi wa Taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela, wakati huu ambapo shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi akiwa katika mapambano dhidi ya maradhi ya mapafu yaliyosababisha kuzorotesha afya yake.

Taarifa toka nchini humo zimeeleza kuwa Obama ameamua kutomtembelea shujaa huyo hospitalini anakopatiwa matibabu mjini Pretoria ili kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.

Tribute: President Obama said his thoughts and those of Americans and people all around the world were with Nelson Mandela and his family
Rais wa Marekani Barack Obama, kulia ni mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
REUTERS/dailymail

Obama amesema kuwa hakuwa na haja ya muda wa kupiga picha na Mandela kufuatia uvumi kwamba angeweza kumtembelea hospitalini kinara huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na mshindi mwenzie wa tuzo ya amani ya Nobeli ambaye amelazwa katika hospitalini kwa zaidi ya majuma matatu sasa.

Obama, ambaye alikutana Mandela mara moja jijini Washington mwaka 2005, amesema kuwa jambo la msingi kwake ni kumpa faraja Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini na ustawi wa familia yake.

Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.

Ziara ya Rais Obama nchini Afrika Kusini haijawa na mvuto kama ilivyotarajiwa kutokana wananchi wa Taifa hilo kuelekeza zaidi macho na masikio yao katika maendeleo ya afya ya kiongozi wao wa zamani.

Via
 kiswahili.rfi.fr

Post a Comment

أحدث أقدم