
Na Mwandishi wetu
BENDI ya African Stars “Wana Twanga Pepeta” kesho Jumapili itazindua
albamu yake 10 ijulikanyo kwa jina la Nyumbani Ni Nyumbani kwenye
viwanja vya Leaders Club huku ikisherehekea miaka 15 tokea kuanzishwa
kwake.
Uzinduzi
huo utapambwa na michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo
timu nane za mpira wa miguu zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano
ijulikanalo kwa jina la ASET Bonanza. Timu hizo zitaongozwa na ile ya
waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point,
Mango, Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.
Mbali
a burudani kutoka kwa Twanga Pepeta, siku hiyo pia kutakuwa na burudani
kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau,
wakongwe wa muziki wa dansi nchini, bendi ya Mlimani Park maarufu kwa
mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.
Mkurugenzi
wa kampuni ya ASET inayomili bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa bendi
inayoundwa na wanamuziki chipukizi au Yosso, Aset Academia nayo itatoa
burudani ya utangulizi katika uzinduzi huo uliodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro, Clouds Media Group, Radio One na CXC Africa.

Asha
alisema kuwa wamejipanga kukoga nyoyo za mashabiki siku hiyo kwani
wameandaa shoo mbali mbali zijulikanazo kwa jina la Twanga 2013 na
nyimbo zao mpya zilizomo kwenye albamu hiyo ambazo ni Nyumbani ni
Nyumbani uliyotungwa na Kalala Junior, Ngumu Kumeza (Ibrahim Mpoyo),
Mwenda Pole (Badi Bakule), Kila Nifanyalo (Jumanne Saidi), Shamba la
Twanga (Greyson Semsekwa na Twanga 2013 ambao ni utunzi wa wanamuziki
wote wa bendi hiyo.
Albamu
nyingine za bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999,
Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe
(2003), Mtu Pesa (2004), Safari (2005),Password (2006), Mtaa wa Kwanza
(2007), Mwana Dar es Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa
mwaka 2011.
Asha
alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha mashabiki wao wapi
walipoanzia (tokea) na wapi wanapokwenda katika muziki wa dansi.
Alisema kuwa kimuziki wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na kupata
mialiko ya kimataifa kama nchi za Ulaya mama Uingereza, Ujerumani,
Uholanzi, Finland, Norway na nyingine nyingi.
إرسال تعليق