Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya
DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na
Marekani mwezi wa tisa mwaka huu.
"yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni
mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu
upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global
promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz
nilipomuuliza kuhu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema
"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa?
إرسال تعليق