Picha
juu na chini ni Afisa uhusiano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa kuhusu siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara
haramu ya madawa ya kulevya kwenye kongamano la vijana kuhusu madawa ya
kulevya mjini Tanga.
Afisa
habari wa kituo cha taarifa cha Umoja wa mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akikabidhi Beji ya utambulisho kwa mmoja wa vijana aliyekaa
miezi sita kwenye nyumba ya mafunzo ya waathirika wa madawa ya kulevya
bila kutumia madawa hayo mjini Tanga katika kituo cha Tanga Sober House.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya vijana wakifuatilia semina ya kupinga
matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya iliyoandaliwa na Kituo
cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na TAYODEA.
Ujumbe
kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam, waandishi wa habari na
watumiaji wa dawa za kulevya walioonyesha nia ya kuacha kutumia dawa
hizo mjini Tanga, ambao wapo kwenye nyumba ya mafunzo ya kuwawezesha
kuachana na dawa hizo (TANGA SOBER HOUSE) iliyopo Tanga. Ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara ya
dawa za kulevya ambayo hufanyika 26 June kila mwaka. Kitaifa maadhimisho
hayo yanafanyika mjini Dodoma.
إرسال تعليق