Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aiomba Mahakama kuu kusogeza mbele tarehe ya Uchaguzi


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Reuters/Philimon Bulwayo
Na Lizzy Anneth Masinga

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepeleka ombi katika mahakama ya juu nchini humo kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi kwa majuma mawili, baada ya shinikizo kutoka kwa Viongozi mbali mbali barani Afrika.

Jaji wa Mahakama kuu nchini Zimbabwe, Patrick Chinamasa ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP kuwa Mugabe amewasilisha nyaraka akitaka kuahirishwa kwa Uchaguzi mpaka tarehe 14 mwezi Agosti kutoka tarehe 31 mwezi Julai mwaka huu.

Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya Viongozi wa Jumuia ya Kusini mwa Afrika kumshinikiza mugabe kuahirisha uchaguzi kwa ajili ya kutoa fursa ya kufanyika mabadiliko ya Kidemokrasia.

Haijajulikana mpaka hivi sasa kama Mahakama kuu itaruhusu kusogezwa mbele kwa uchaguzi mkuu nchini humo.

Uchaguzi ujao utampata mrithi wa Serikali ya Shirikisho, iliyoundwa miaka minne iliyopita kama suluhu ya machafuko ya kisiasa nchini Zimbabwe.

Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na Mugabe walitangaza kuanza mchakato wa mabadiliko kwa kutoa uhuru kwa Vyombo vya Habari, kutowahusisha Wanajeshi na Polisi katika maswala ya Siasa na kuhakikisha kuwepo kwa hali ya Uwazi wakati wa Uchaguzi, mabadiliko yanayotazamiwa kufanyika kabla ya Zoezi la kupiga kura.

Viongozi wa Mataifa 15 wa jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC mwishoni mwa Juma walimshinikiza Mugabe kurudi mahakamani na kuomba kuahirisha uchaguzi. Via kiswahili.rfi

Post a Comment

أحدث أقدم