STEPS KUTOA TUZO ZA FILAMU JUMAMOSI


Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited Jumamosi  itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania.
Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu.
Silondwa alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike, muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.
Silondwa alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.
Alisema kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.
“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.
Alisema kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps Solar pekee

Post a Comment

أحدث أقدم