Sehemuambapo kisima kimechimbwa |
Kisima chenyewe kinavyoonekana |
Kilindo (kulia) akizungumza na baadhi ya wanakijiji pamoja na wafanyakazi wa TBL wakati wa makabidhiano ya kisima hicho. |
Mmoja wa viongozi wa kijij cha Isnura akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu. |
Baadhi ya wanakijiji wakishuhudia makabidhiano hayo |
BAADA ya Wananchi wa Kijiji cha Isnura kata ya
Mawindi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuteseka kwa zaidiya miaka mitano
kutokana na ukosefu wa maji safi na salama hatimaye neema yawaangukia baada ya
kujengewa kisima kitakachozalisha maji miaka yote.
Akizungumzia adha ya Maji iliyokuwa ikiwasumbua
wananchi hao, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Josphine Ndimilage alisema tatizo hilo
lilianza mwaka 2008 baada ya idadi kubwa ya watu kuongezeka katika Mji wa
Rujewa na kufanya maji yaliyokuwa yameletwa na kampuni ya Danida kupungua.
Alisema baada ya watu kuongezeka maji yalianza
kusumbua na kufikia hatua ya kugawana maji ambapo kijiji hicho kilikuwa
kikipata mara moja kwa wiki hivyo kluwalazimu wananchi kutumia maji machafu
yaliyotwama makorongoni maji ambayo yalikuwa yakitumiwa na mifugo.
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho
umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 41
ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika Tanki
kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Sheria wa Kampuni ya
Tbl, Stephen Kilindo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Isnura alipokuwa
ametembelea maendeleo ya ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia Tisini
aliwaasa Wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kudumu milele.
Alisema Kampuni yake imechimba kisima hicho
kutokana na Maombi ya wananchi wa eneo husika yatokanayo na mahitaji ya maji,
uwepo wa magonjwa, idadi ya watu na mwitikio wa wananchi wa kupokea mradi tangu
katika hatua za awali jambo ambalo liliitikiwa vizuri na wakazi wa kijiji cha
Isnura.
Alisema kutokana na mradi huo ambao utawanufaisha
zaidi ya wakazi 4000 unakabiliwa na changamoto ya Nishati kwa ajili ya
kupandisha maji kutoka chini hadi kwenye tanki ambapo Mkurugenzi aliwataka
wanakijiji hicho kuchukua jukumuhilo na siyo kutegea ili wafadhili wafanye wao
wenyewe.
Kilindo alisema Kampuni inafanya kazi ya kutoa
misaada ili kuisaidia Serikali kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi
ikiwa ni pamoja na kurudisha shukrani kwa kile kinachovunwa katika rasilimali
za nchi kwa kutoa misaada mbali mbali katika jamii.
Aliongeza kuwa mradi huo haupo kisiasa na
kuwaomba wananchi wamwandae kiongozi wa kuzindua mradi huo ambye hatakuwa
mwanasiasa wa chama chochote cha Siasa uzinduzi ambo utafanyika Juni 27, Mwaka
huu baada ya kukamilika kabisa.
Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga kisima
hicho Moses Francis Lujaji kutoka kampuni ya Water Family Co.Ltd alisema
tangu mradi huo uanze haujachukua muda mrefu kutokana na wananchi kuonesha
ushirikiano na msaada kwa mafundi.
Aidha aliongeza kuwa baada ya kufanikiwa kuchimba
kisima hicho chenye urefu wa Mita 80 walikuta maji mengi ambayo yakitumiwa
vizuri hayataweza kukauka milele yote na kuongeza kuwa tayari Maabara ya
Serikali imeshaidhinisha maji hayo kuwa yanafaa kwa matumizi ya binadamu
baada ya kupimwa.
Picha Na:- http://richard-mwaikenda.blogspot.com/
|
Post a Comment