TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MILIONI 41 KIJIJI CHA ISNURA, MBARALI, MKOANI MBEYA


 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake  wakifurahia maji yanayotoka katika kisima walichosaidia kijijini isnura, wilayani Mbarali, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni kijijini hapo.
Sehemuambapo kisima kimechimbwa
Kisima chenyewe kinavyoonekana
Kilindo (kulia) akizungumza na baadhi ya wanakijiji pamoja na wafanyakazi wa TBL wakati wa makabidhiano ya kisima hicho.
Mmoja wa viongozi wa kijij cha Isnura akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu.
Baadhi ya wanakijiji wakishuhudia makabidhiano hayo
Mkurugenzi waUhusiano na Sheria wa Kampuni ya Tbl, Stephen Kilindo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Isnura alipokuwa ametembelea maendeleo ya ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia Tisini aliwaasa Wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kudumu milele.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Isnura Josphine Ndimilage amesema tatizo la maji lilianza mwaka 2008 baada ya idadi kubwa ya watu kuongezeka katika Mji wa Rujewa na kufanya maji yaliyokuwa yameletwa na kampuni ya Danida kupungua.


BAADA ya Wananchi wa Kijiji cha Isnura kata ya Mawindi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuteseka kwa zaidiya miaka mitano kutokana na ukosefu wa maji safi na salama hatimaye neema yawaangukia baada ya kujengewa kisima kitakachozalisha maji miaka yote.
  
Akizungumzia adha ya Maji iliyokuwa ikiwasumbua wananchi hao, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Josphine Ndimilage alisema tatizo hilo lilianza mwaka 2008 baada ya idadi kubwa ya watu kuongezeka katika Mji wa Rujewa na kufanya maji yaliyokuwa yameletwa na kampuni ya Danida kupungua.
Alisema baada ya watu kuongezeka maji yalianza kusumbua na kufikia hatua ya kugawana maji ambapo kijiji hicho kilikuwa kikipata mara moja kwa wiki hivyo kluwalazimu wananchi kutumia maji machafu yaliyotwama makorongoni maji ambayo yalikuwa yakitumiwa na mifugo.
  
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 41  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Sheria wa Kampuni ya Tbl, Stephen Kilindo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Isnura alipokuwa ametembelea maendeleo ya ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia Tisini aliwaasa Wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kudumu milele.
  
Alisema Kampuni yake imechimba kisima hicho kutokana na Maombi ya wananchi wa eneo husika yatokanayo na mahitaji ya maji, uwepo wa magonjwa, idadi ya watu na mwitikio wa wananchi wa kupokea mradi tangu katika hatua za awali jambo ambalo liliitikiwa vizuri na wakazi wa kijiji cha Isnura.
  
Alisema kutokana na mradi huo ambao utawanufaisha zaidi ya wakazi 4000 unakabiliwa na changamoto ya Nishati kwa ajili ya kupandisha maji kutoka chini hadi kwenye tanki ambapo Mkurugenzi aliwataka wanakijiji hicho kuchukua jukumuhilo na siyo kutegea ili wafadhili wafanye wao wenyewe.
  
Kilindo alisema Kampuni inafanya kazi ya kutoa misaada  ili kuisaidia Serikali kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kurudisha shukrani kwa kile kinachovunwa katika rasilimali za nchi kwa kutoa misaada mbali mbali katika jamii.
  
Aliongeza kuwa mradi huo haupo kisiasa na kuwaomba wananchi wamwandae kiongozi wa kuzindua mradi huo ambye hatakuwa mwanasiasa wa chama chochote cha Siasa uzinduzi ambo utafanyika Juni 27, Mwaka huu baada ya kukamilika kabisa.
Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga kisima hicho Moses Francis Lujaji kutoka kampuni ya Water Family Co.Ltd  alisema tangu mradi huo uanze haujachukua muda mrefu kutokana na wananchi kuonesha ushirikiano na msaada kwa mafundi.
Aidha aliongeza kuwa baada ya kufanikiwa kuchimba kisima hicho chenye urefu wa Mita 80 walikuta maji mengi ambayo yakitumiwa vizuri hayataweza kukauka milele yote na kuongeza kuwa tayari Maabara ya Serikali  imeshaidhinisha maji hayo kuwa yanafaa kwa matumizi ya binadamu baada ya kupimwa.

Post a Comment

أحدث أقدم