
Star wa timu ya taifa ya Senegal na klabu ya Newcastle United ya ligi
kuu ya England Demba Pappis Cisse hatimaye ameonekana kusalimu amri na
kukubali kuvaa jezi ya Newcastle ambayo itakuwa na nembo ya mdhamini
mkuu wa Klabu hiyo ambaye ni kampuni ya Wonga.
Cisse ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Senegal amekubali kuvaa
jezi hiyo baada ya kugoma kutokana na sababu za imani ya dini yake ya
uislamu ambayo haiafiki masuala ya riba kwenye mikopo au biashara, na
ilifikia hatua ya kupewa adhabu ya kufanya mazoezi mwenyewe na kuachwa
na klabu hiyo wakati wenzie walipoenda nchini Ureno kufanya mazoezi ya
kabla ya msimu ambapo ilidhaniwa kuwa nyota huyo angeweza hata kufukuzwa
kutokana na msimamo wake.
Siku chache zilizopita wadakuzi wa magazeti ya England walimnasa
Cisse akiwa ndani ya Casino akiwa amekaa kwenye meza ya kucheza kamari
jambo ambalo liwafanya watu washindwe kuelewa nini kinaendelea kwani
kamari kama ilivyo kwa masuala ya riba ni haramu kwa Waislamu.

Picha inayomuonyesha Cisse akiwa kwenye meza ya Kamari ndani ya Casino.
Wonga ni kampuni ambayo inafanya biashara ya kukopesha watu ambapo
mikopo inayotolewa na kampuni hiyo inalipwa kwa kutoza riba ya juu jambo
ambalo Cisse kama muumini safi wa dini ya kiislamu anapingana nalo.
Hata hivyo suala hilo limemalizwa baada ya Pande zote kukaa chini na
kuzungumza na kupata ufumbuzi kwenye Kikao kilichoongozwa na viongozi wa
chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA na sasa Cisse atavaa
jezi za Wonga kama mchezaji mwingine yeyote wa Newcastle.

Mmoja wa wachezaji waislamu wa Newcastle Mousa Cissoko akiwa amevaa jezi ya Wonga.
Story za Michezo hapa millardayo.com ni kwa nguvu ya Benki Ya NMB….
waliozitandaza ATM Machine zaidi ya 500 kote Tanzania kwa ajili yako,
toa pesa popote na wakati wowote
إرسال تعليق