
Proxy War au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu
nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na
nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na
mapambano yalitokea katika nch zote mbili.
Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B
katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika
nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka
askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka
askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na
serikali ya nchi C.
Naomba ieleweke kuwa mie sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet
of doom.' Ninachoongelea hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye
mapigano yanayoendelea nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo
na kikundi cha waasi cha M23.
Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa kushirikiana na Malawi na Afrika
Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Lakini kuna taarifa
kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na Rwanda (kama ni kweli au la,mie
sina hakika...lakini lisemwalo lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si
Kenya au Msumbiji?)
Sasa tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku
za hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa
"atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha mtandike" kuna
uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC.
Kwanini ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au
Tanzania kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali.
Lakini nchi hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia
mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha
Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23
(wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)
Vyovyote itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee
kwa gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of
War), Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na
kifo, barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."
Kuna wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa
kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU,
ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu
(wapelelezi) wa ndani na wa nje.Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda
wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile
ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo
tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi
wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50? Soma hapa http://suntzusaid.com/book/13 kufahamu
zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN
TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao
kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)
Anyway, kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa
majanga.Ningependa sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu
lao haraka na kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu
PROXY WAR ni uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.
Post a Comment