Ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja toka staa wa Bongo Luca Mkenda aka Mr Nice
apoteze nafasi ya kufanya kazi na label ya GrandPa ya Kenya kwa shutuma
za uvivu, kushindwa kutoa ushirikiano na ukiukaji wa mkataba hatimaye
mlango mwingine umefunguka kwa nyota huyo wa ‘Kikulacho’.
Mr Nice ambaye bado yuko Kenya anatarajia kujiunga na label nyingine nchini humo ‘Candy Records’
ambayo ina miezi michache toka ianzishwe. Kwa mujibu wa CEO wa label
hiyo John Kariuki aliyekuwa akizungumza katika ufunguzi rasmi wa label
hiyo jijini Nairobi, alisema wako katika hatua za mwisho kukamilisha
mpango wa Mr Nice kusain mkataba nao kama ilivyoripotiwa na Niaje.
Label hiyo tayari imesha wasain wasanii kadhaa wa Afrika Mashariki
akiwemo hit maker wa ‘Ulofa’ Top C wa Tanzania, pamoja na wengine kutoka
Kenya

إرسال تعليق