Wanasayansi
wametengeneza kisu cha upasuaji ‘intelligent surgical knife’ chenye
uwezo wa kugundua kwa sekunde kama sehemu inayokatwa katika mwili wa
binadamu wakati wa upasuaji ina kansa ama laa.
Kisu hicho kilichobuniwa na watafiti wa Imperial College huko
London, Uingereza kitawawezesha madaktati kufanya upasuaji wenye uhakika
zaidi kwa wagonjwa wao.
Kwa mujibu wa wataalam upasuaji mara nyingi huwa ni vigumu kujua kwa
kuona mwisho wa uvimbe hivyo ni ngumu kwa surgeon kufahamu mahali
anapotakiwa kuishia kukata, hivyo wakati mwingine cell za kansa huachwa
bila kuondolewa na kuhitaji upasuaji mwingine kwa mgojwa baadaye.
Kisu hicho kipya kilichopewa jina la “iknife” yaani (Intelligent
Knife) kimetengenezwa kukabiliana na tatizo kama hilo na katika
majaribio ya kwanza yaliyofanywa, kilitoa majibu sahihi kwa wagonjwa 91
kwa mujibu wa watafiti wa Imperial College London waliotoa ripoti yao
Jumatano wiki hii.
Mgunduzi wa kifaa hicho Zoltan Takats wa Imperial College alisema
malengo yake yalikuwa ni kufanya majaribio kwa wagonjwa kati ya 1000
mpaka 1500 wanaosumbuliwa na aina tofauti za kansa, na mchakato huo wa
majaribio unategewa kuchukua kati ya miaka 2 au 3 kabla iknife
haijawasilishwa kwa mamlaka zinazohusika kupitisha iingie katika
biashara.
Video:AlJazeera
إرسال تعليق