Laico Regency |
Kanisa
jipya limeanzishwa nchini Kenya kwa lengo la kutoa huduma ya neno la
Mungu kwa aina fulani tu ya watu ambao ni watu maarufu ‘celebrities’
pamoja na watu wenye pesa. Kanisa hilo limepewa jina la The All-Star Church.
Kwa mujibu wa taarifa ya Cate Mukei katika mtandao The-Nairobian,
kanisa hilo ambalo limezinduliwa Jumapili iliyopita (July 7) litakuwa
likitumia ukumbi wa hotel yenye hadhi ya nyota 5 Laico Regency iliyoko
Nairobi, na linawalenga wanamuziki, wanamichezo mastaa, waigizaji,
wanasiasa wa ngazi za juu, na watu wa Corporate.
Pasta mkuu wa ‘The All-Star Church’ Catherine Munene, ameuambia
mtandao wa The Nairobian kuwa, hawatafuti watu maarufu wala hawawawindi,
isipokuwa wanawahimiza kwenda kuabudu katika kanisa hilo sababu wanatoa
huduma inayoendana nao. “We are not looking for celebrities or
hunting for them. But we are encouraging them to come as we are offering
what is relevant.”
Pia pasta huyo mwanamke alikanusha uvumi kuwa wamepewa ukumbi huo wa hotel bure na kusisitiza wanaulipia pesa nyingi “We
are paying a lot of money which of course I cannot disclose. Please
don’t listen to rumours that could destroy my church. I know media
houses destroy churches and if The Nairobian does this we will deal with
you. We are very powerful,” Alisema pasta Munene.
Kazi kwenu mastaa wa Nairobi.
Picha: Standard Digital
Post a Comment