RIWAYA: ROHO MKONONI 19

Photo: RIWAYA: ROHO MKONONI
MTUNZI: George Iron Mosenya

SEHEMU YA KUMI NA TISA

Wakati Isaya anafika nyumbani kwake. Yeye Fonga alikuwa njiani kuelekea Machimbo kuonana na Joyce. Kuna jambo muhimu ambalo Joyce alihitaji kujadili naye, hata Fonga naye alihitaji kumweleza Joyce juu ya maendeleo  ya mchakato huo ambao kwa wakati huo ulikuwa mchakato wa kumrejesha Betty uraiani akiwa hai.

Walikutana maeneo ya Buguruni. Fonga hakutaka kukutana naye nyumbani kwa dada yake kwa sababu kwa kufanya hivyo angeweza kuongeza tatizo juu ya tatizo. 
Tayari alishatambua kuwa kuna watu wabaya nyuma yake wanamfuatilia yeye na Joyce. Hakujua sababu lakini alichukua tahadhari mapema.
Kama ilivyo ada akamwelekeza Joyce aina ya mavazi ambayo alitakiwa kuvaa. Naye akatii!!
Katika mgahawa mmoja akaonekana msichana akiwa na baibui akizungumza na mwanaume!!
Fonga na Joyce!!
Mazungumzo haya yalihusiana na hatma ya maisha ya Joyce na muafaka wa Betty huko alipo.
Fonga hakukurupuka kujibu badala yake akamuuliza swali.
“Joy!! Unajua kuwa roho ya Betty ipo mikononi mwako?”
“Una maana gani wakati wewe umenihakikishia kuwa nitarejea shuleni na Betty atapatikana?” aliuliza kwa hamaki kidogo.
“Joyce!! Kuna jambo lolote ambalo unanificha labda kuhusiana na tukio hili, yaani lolote hata kama ni la kihisia wewe nieleze mimi na hapo nitajua wapi wa kuanzia sawa mamii” Fonga alisihi huku akiyatazama macho ya Joyce kutokea katika nikabu!!!
“Mi kwa kweli sijui lolote kuhusiana na  Betty, zaidi ya hayo yote niliyokwisha kueleza zamani.” Alijibu Joyce katika namna ya kukwazika na kukata  tamaa.
Fonga alimung’unya midomo  yake huku akitikisa mguu wake wa kulia kama  vile amegundua jambo tayari. 
Naam! Fonga alikuwa akijaribu kufikiri mambo kadha  wa kadha  ambayo yanaweza kusababisha Joyce na Betty wawe matatani. Mwanzoni alitupa karata yake katika mambo ya pesa lakini kwa mtazamo  tu Joyce hakuwa na  pesa, lakini alikuwa na urembo ambao ungeweza kumletea pesa nyingi tu.
Alipofikiria jambo hili akajiuliza, kwanini hana pesa?
Jibu sahihi kutokana na hisia zake likawa, amegoma  kutumia urembo wake kujipatia pesa. Kwa hiyo kuna  uwezekano mkubwa kuwa amewakataa wanaume wengi sana wenye pesa zao, jambo hili huenda limewakasirisha na sasa wanalipiza kisasi.
Sasa hawa wanaume ni akina nani? Akajiuliza kisha akamtazama tena Joyce.
“Nani alikuwa mpenzi wako siku za nyuma?  Hapa chuoni!”
“Sijawahi kuwa na mpenzi mimi,  mbona waniuliza maswali hayo jamani?” alifoka kidogo.  Fonga hakujali.
“Ina maana tangu uje hapa chuo hujajihusisha na mapenzi?”
“He! Fonga unataka nikuchoree nd’o uamini ama maana nasema hunielewi.” Alikazia Joyce.
Fonga hakutaka kuendelea kuhoji, akaamua kutupa karata nyingine ambayo Joyce bila kujua kuwa ni karata ileile kama ya awali alijikuta akiipokea vizuri.
“Joyce, ujue tunahitaji pesa ya ziada katika jambo hili, kuna maadui wametuzunguka. Tunachokitafuta sasa sio tu kupatikana kwa Betty, bali tupo katika kuitafuta amani yetu pia. Maana kwa sasa hata serikali inaamini kuwa sisi ni waarifu, hakuna anayetuamini hata mmoja. Hivyo ni sisi tunatakiwa kutafuta kuaminiwa na turejee katika maisha yetu ya awali. Nikisema jambo hili lazima mimi na wewe tushirikiane namaanisha kuwa tusifichane lolote lile, nimekuamini nikaamua kukusaidia nawe niamini kama nikuaminivyo!!” alihitimisha Fonga.
“Nakuelewa sana Fonga na ninajitahidi sana kuwa mkweli kwako. Hakuna  jambo ambalo ninakuficha.” Alisisitiza Joyce kwa kujiamini.
Fonga aliisoma akili yake na kugundua alikuwa ni mtu wa kukata tamaa upesi sana. Akatikisa kichwa kumsikitikia.
“Ehe! Ulikuwa nawe una jambo gani la kunishirikisha.” Fonga aliuliza kivivu vivu.
“Ahaa! Ni kuhusu kutafuta mtu mwenye nyadhifa serikali aweze kutusaidia katika jambo hili ama waonaje wewe.” Alisema Joyce.
“Tunampata wapi mtu huyo sasa, na unajuaje kama mtu anayetukosesha amani naye ni wa huko serikalini? Huoni kama unataka kujikabidhi katika domo la mamba kiulaini.” Fonga alijibu kwa utulivu!! Maneno yakamuingia Joyce akilini.
Akakiri tena kuwa Fonga alikuwa mtu wa aina yake, alikuwa na akili ya ziada. Uwezekano huo wa kupata mtu wa serikali ambaye atawasaidia ukafutwa rasmi. Wakaendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale kisha wakaagana.
Fonga akizidi kumsisitiza Joyce kuwa amuachie mambo yote yeye na kila kitu kitaleta majibu ya uhakika.

JOYCE alihangaika kuupata usingizi kwa siku ile, alikuwa ameichoka hali ile ya kukosa uhuru wake aliokuwa ameuzoea.
Akafikiria sana na kuona kuwa Fonga hana lolote la kumsaidia zaidi ya kuzungusha  maneno yenye ushawishi. Kitu ambacho Joyce hakukipinga ni kuwa Fonga alikuwa ana nia lakini huwezo hakuwa nao. Uwezo wa kupambana na adui asiyefahamika.
Joy akaukumbuka usemi wa akili ya kushikiwa changanya nay a kwako, akaanza kulitafuta jibu la ni kwa namna gani anaweza kujiweka huru.
Akafumba macho yake mara akakumbuka kisanga cha takribani mwaka mmoja uliopita.  Kisanga ambacho hakutaka kukikumbuka katika maisha yake japo kiligoma kujifuta akatika akili yake siku  zote licha ya kupitia mengineyo mengi. 
Hiki kilikuwa kisa ambacho aliamua kuishi nacho kwenye akili yake tu!! Hata rafiki yake wa damu kabisa Betty, hakuwahi kumshirikisha juu  ya jambo hilo.
Hakumshirikisha kwa sababu hakutaka kulikumbuka kamwe!!

MISS CHUO KIKUU, 2007

WAHKA wa kutawazwa kuwa mrembo wa chuo kikuu ulikuwa umempanda, sifa kemkem alizokuwa amemwagiwa zilimfanya azidi kupagawa na kutamani kuonyesha kuwa anaweza. Walikuwa warembo ishirini waliokuwa wakichuana  vikali kuwania taji hilo.
Jina lake lilitajwa midomoni mwa wadau wengi wa mambo ya urembo kama mshindi mtarajiwa. Jambo hilo lilimtia hamasa sana! 
Akamfikiria mpinzani wake mkuu aliyeitwa Monica, akatabasamu na kuifikiria siku ambayo atavikwa taji la urembo huku Monica akisimama pembeni kama mshindi wa pili.
Monica nd’o alikuwa mpinzani wake haswaa!!

Kambi  ya Joyce Kidoti walimtegemea kijana Fonga kwa ajili ya kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka kambi pinzani, hivyo kuwawezesha kujipanga vyema wasitetereke.
Siku nne kabla ya mpambano ndipo kikatokea kisanga hicho cha aina yake. Joyce alipokea simu kutoka kwa mwanaume aliyejiita Bernad Karama. Alijitambulisha kama jaji mwenye ushawishi na aliyepewa mamlaka zaidi katika shindano hilo la ulimbwende. Joyce alimuuliza iwapo anamuhitaji kwa mambo binafsi ama ni kwa shughuli hiyo iliyopo mbele yao.
Bwana Karama akamweleza kuwa ni shughuli ya kiofisi zaidi na ilikuwa lazima waonane jioni hiyo hiyo.
Joyce akakubali wito huku akijionya kuwa iwapo patakuwa na jingine la ziada basi atakataa.

Akafunga safari hadi maeneo ya Changanyikeni, ni huku bwana Karama alikuwa amemuelekeza. Kwa sababu mshiriki alikuwa ni yeye basi hakulazimika kwenda na mtu mwingine.
Majira ya saa moja usiku alikuwa nyumbani kwa Karama.
Bwana huyu akamueleza kuwa amelishikilia taji la mrembo wa chuo kikuu, na ni yeye atakayeamua kumpatia aidha yeye Joyce ama kumpatia Monica.
Joyce hakuelewa mara moja bwana yule anamaanisha nini. Lakini kadri alivyozidi kujipambanua ndipo walipolifikia lengo.
Karama alikuwa anahitaji penzi la Joyce ili aweze kumpatia ushindi!!
“Joyce, acha kuwa kamamtoto mdogo. Ni nani atakayejua kuwa jambo hili limetokea unadhani? Kumbuka kuwa unao mashabiki wengi sana huenda kuliko Monica lakini ni mimi nitakayetoa kura kuu ya mwisho.” Alisisitiza Karama huku akionekana kumaanisha alichokuwa akisema.
Joyce alikuwa kimya akitafakari juu ya maneno ya Karama na kisha kujiuliza ataweza vipi kuzihimili kelele za mashabiki wa Monica iwapo atashindwa katika mchuano huo.
Akafikiria mengi na kisha kujikuta katika mtego wa Karama. Mtego ambao aliamua kuubakisha kama siri yake ya maisha kwa sababu hakutaka kila mtu aujue udhaifu wake kutokana na kelele za mashabiki.
Joyce akakubaliana na Karama  usiku uleule.
Wakati Karama akidhani kuwa Joyce ni msichana kama wasichana wengine wenye uzoefu katika mambo hayo mbele yake, alijikuta katika wakati mgumu wa kupambana na Joyce ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya mapenzi.
Karama akaitoa bikra ya Joyce!!
Maajabu!! Maajabu asilani!

SIKU ya mpambano, jaji Karama alikumbwa na dharula hakuweza kuhudhuria mpambano huo wa kukata na shoka. Mchuano wa ulimbwende.
Hali ya kutomuona Karama  katika meza ya waamuzi ilimtia Joyce katika mashaka na kujikuta akikosa  lile tabasamu lake halisi. Akakosa uchangamfu na mwisho wa mpambano.
Monica akaamuriwa kuwa mshindi!!
Joyce Kidoti akiikamata namba mbili kwa masikitiko makubwa.
Hakumweleza mtu yeyote juu ya jambo lililotokea kati yake na Karama.

Baada ya jumamoja ndipo usumbufu ulipoanza, Karama akarejea tena katika maisha yake. Sasa alikuwa akitaka kumuoa  Joyce, jambo lililopingwa vikali na binti huyo. Alipinga haswa.
Karama  hakuchoka kubembeleza, alisisitiza kuwa yupo tayari kumtambulisha kwa wazazi wake na kisha kumchumbia kisha amuache akiwa anasoma. Lakini bado Joyce akuvutika na mwanaume huyo aliyemtoa usichana.

Sasa Joyce amekwama, anakumbuka kuwa yule jaji Karama sasani mbunge. Ana heshima kubwa katika jamii, na kutokana na tatizo alilonalo anaamua kumtafuta ili aweze kumsaidia na amani iweze kurejea tena.
Anaitafuta namba yake na  kuipata kupitia watu kadhaa aliofahamiana nao.
Anampigia simu na kujitambulisha, Karama anazungumza kwa shangwe sana na asiamini kile alichokuwa anakisikia.
Wakapanga kukutana!!
Joyce mwenye matatizo tena dhidi ya mbunge Karama Benard.

****

FONGA alipokea simu kutoka kwa dada yake, Zubeda. Majira ya saa nne asubuhi. 
“Fonga, huyu mkeo ameondoka muda si mrefu hapa na hajaniaga bali amesema anawahi kurudi.” Dada mtu alimpa taarifa Fonga kama ambavyo alikuwa ameelekezwa kuwa iwapo ataondoka basi apewe taarifa upesi.
Fonga akakurupuka  kutoka kitandani, akajipongeza kwa machale yake sahihi. 
Fonga ambaye alikuwa nyumba ya jirani kabisa na mahali anapoishi dada yake alivaa shati lake na kisha akaingiza miguu yake katika makubadhi. Akanyata na kutoka nje akiwa ametinga kofia ya pama.
Ilikuwa ngumu kumtambua, kwa mbali akamuona Joyce akitembea upesi upesi. Fonga akasikitika kisha akatabasamu, alikuwa anaufurahia mchezo ambao alikuwa anaenda kuucheza.
Mchezo wa kufungiana tela!!
Upesi akachumpa katika taksi ambayo alikuwa ameikodi kwa shughuli za hapa na pale hasahasa katika tukio zima la kumsaka mbaya wao.
Akatazama kwa makini Joyce naye akiwa na baibui lake akijiweka katika taksi mojawapo. Ilipoanza kuondoka naye akaingiza gari barabarani na kuanza kumfuatilia yule binti mahali ambapo alikuwa anaelekea.
Safari yao ikaishia katika hoteli ya ‘Rombo Green View’ iliyopo maeneo ya Sinza Legho. Fonga akaegesha gari yake na kisha kuingia katika hoteli hiyo na kujiweka katika kona moja matata ambayo hakuna ambaye angeweza kutambua alikuwa na jambo gani.
“Niletee Safari mbili za baridi.” Alitoa oda kwa muhudumu. Wakati huo macho yake yapo kwa Joyce ambaye alikuwa akiangalia saa yake kila mara.
Amenifurahisha sana kuvaa kama nilivyomwambia!! Fonga akajisemea huku akimtazama Joyce aliyekuwa hana habari kabisa.
Mara baada ya dakika kadhaa lilifika kundi dogo la wanaume watatu. Wakaangaza huku na kule, Fonga naye akawatazama kwa jicho la wizi wizi. Waliporidhika mmoja wao akapiga simu.
Na hapo likatokea tukio la kuogofya!!
Akaingia mwanaume ambaye alikuwa nakila dalili ya maisha ya kifahari. Akapiga hatua moja baada ya nyingine na kuifikia meza aliyokuwa ameketi Joyce Kidoti. Bila shaka alikuwa ameelekezwa kwa njia ya simu tayari juu ya namna gani binti huyu alikuwa amevaa.

Damu ya Fonga ni kama iliongeza mwendo kutokana  na mapigo ya moyo kuongeza kasi yake. Macho yake yalikuwa yanatazamana na mwanaume ambaye alikuwa akimchukia kupita wote duniani!! Mwanaume katili aliyetia doa historia ya maisha yake.
Mzee Beka!!
Mwanaume aliyemtupa jela kwa miezi tisa bila kuwa na kosa. Mwanadamu mbaya asiyekuwa na huruma!!
Fonga alitaka kuinuka na kumvagaa lakini akajionya kuwa mvumilivu na kutazama ni kipi kinaendelea baina ya wawili wale.
Fonga alimtazama Beka huyu tofauti kabisa na yule wa zamani, huyu alikuwa nadhifu zaidi. Na alionekana kuimarika zaidi ya awali.
Kwa mara ya kwanza Fonga anamuona Beka ambaye awali walipoonana alikuwa akiitwa Bernad Kamara, sasa alikuwa amelifupisha jina lake kamili na kulifanya kuwa moja!!
Sasa anaitwa Beka!!!

Wakati akijiuliza ni kipi afanye, mara alishtukia anaguswa begani. Alipogeuka akakutana na mwanaume akiwa ndani ya vazi la suti. Alikuwa akitabasamu na macho yake yalizibwa na miwani nyeusi ya jua.
Kwa wepesi wa akili yake, akatambua kuwa kuna jambo. Alipokazia macho mikono ya yule bwana katika suti yake akaona umbo ambalo halikuwa geni vilevile machoni.
Mtutu wa bunduki!!!
“Habari bwana!!” yule mtu alimsabahi huku akimpa mkono. Fonga akastaajabu, kasha akkiri kuwa akiwa lelemama huo ni mwisho wa mchezo.
Fonga akatambua kuwa alikuwa anakabiliana na mzee Beka kwa mara nyingine katika maisha yake. Mchezo wa kwanza alipoteza vibaya….na huu nao dalili ikaanza kuonekana awali….
Amejuaje uwepo wangu hapa!! Alijiuliza huku akiwa hajafanya maamuzi…..
Jicho moja likamtazama Joy akishikwa shikwa bega na mzee Beka, jicho jingine likageuka na kukutana na kijana mwenye mtutu wa bunduki!!!
Hatari!!!

***JOYCE amejipeleka kwa BEKA ………nini kitajiri??
**Kumbe FONGA amewahi kumtambua BEKA kabla ya siku hiyo??
***Akiwa hajajua ni kipi afanye anajikuta akikabiliwa na balaa jingine..
JE HUU ND’O MWISHO WA MCHEZO??

***ITAENDELEA!!!!

RIWAYA: ROHO MKONONI

Post a Comment

Previous Post Next Post