Hii ndio kampuni iliyotangaza 'bifu' kali na Chris Brown( sababu ambazo hazijatajwa )


Moja wa wadhamini wa show kubwa kabisa ambayo ita-happen huko Canada mwezi ujao, wamejitoa katika mpango huo mara baada ya kugundua kuwa Msanii Chris Brown ameongezewa katika listi ya wasanii watakaoperform.

Kampuni hii maarufu ya Rogers Communication haijatoa sababu yoyote ya ndani kuhusiana na ni kwanini wamejiondoa katika udhamini wa tamasha hili ila kwa mujibu wa moja ya wasemaji wa kampuni hii, uamuzi wao ni kutokana na msimamo waliojiwekea kuwa, hawatajihusisha na wala hawataki kujihusisha na shughuli yoyote ambayo kwa namna moja ama nyingine inamhusisha Chris Brown.


Onyesho hili litafanyika huko Canada Halifax August 31 mwaka huu.

Post a Comment

أحدث أقدم