Na Sabina
Chrispine Nabigambo
Marekani imetoa wito kwa jeshi la Misri
kumwachia huru rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi, huku makumi kwa
maelfu ya wafuasi wake wakiapa kuendelea kupigana kwa ajili ya kurejeshwa kwake
madarakani.
Msemaji wa Ikulu Jen Psaki amesema kuwa
Marekani imekubaliana na wito wa awali wa Ujerumani kuhusu kuachiwa huru kwa
Morsi na sasa inatoa wito huo huo hadharani.
Morsi ambaye aliondolewa madarakani mnamo July
3 amehifadhiwa mahali salama kwa mujibu wa viongozi wa mpito wa serikali ya
Misri na hajaonekana hadharani tangu kupinduliwa kwake.
Psaki amesema kuwa Washington inataka
kukomeshwa kwa vikwazo dhidi ya wapi alipo Mohamed Morsi wakati Ujerumani
imependekeza taasisi inayoaminiwa kama vile Kamati ya Kimataifa ya Msalaba
Mwekundu ICRC iruhusiwe kumfikia.
Via kiswahili.rfi.fr
إرسال تعليق