Majangili wenye silaha waua askari wawili wa wanyamapori


Askari wawili wa wanyamapori (KWS) wameuawa nchini Kenya katika matukio mawili tofauti ya kukabiliana na uwindaji haramu kwenye hifadhi ya maliasili ya Kipini iliyoko wilaya ya Tana River nchini humo.
Afisa uhusiano wa KWS Paul Udoto amesema, jangili mmoja pia ameuawa katika mapigano hayo, na silaha aina ya AK 47, bunduki 3, na risasi 208 zimekamatwa. Amesema tukio la kwanza lilitokea wakati askari wa wanyamapori waliokuwa doria kukutana na watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa walikuwa wanawinda tembo.
Mapigamo mengine makali kati ya askari hao na majangili yalizuka saa sita baadaye na kusababisha kifo cha askari mwingine. Hakuna taarifa zozote kama kuna majangili waliojeruhiwa katika mapigano hayo.

Chanzo: CRI

Post a Comment

أحدث أقدم