Mojawapo ya mashambulizi ya mabomu yaliyowahi kutekelezwa mjini Baghdad mwaka 2013
Reuters/Wissm al-Okili |
Mashambulizi ya mabomu yaliyolenga ngome za watu wa jamii ya
kishia yametikisa nchi ya Iraq jumatatu hii na kusababisha mauaji ya
watu takribani 48 na kujeruhi wengine zaidi ya 150, Maofisa wa usalama
na Madaktari wamethibitisha na kubainisha kuwa idadi hiyo inafanya idadi
ya vifo vya mashambulizi kwa mwezi huu wa Julai kuwa zaidi ya 780 idadi
ambayo ni kubwa zaidi kufikiwa katika kipindi cha mwezi mmoja.
Milipuko ya mambomu 11 ilishambulia maeneo tisa tofauti mjini
Baghdad, saba kati yao ikielekezwa kwenye eneo waishio waumini wa Kishia
na mengine iliyosalia katika eneo la Mahmudiyah Kusini mwa mji mkuu wa
nchi hiyo.
Mashambulizi ya hii leo limekuja siku moja baada ya watu wengine 14
wakiwamo polisi wa kikurdi 9 kuuawa katika shambulio mjini Tuz Khurmatu
kaskazini mwa nchi hiyo.
Barabara na miundombinu mingine imeripotiwa kuendelea kuzorota kutokana
na mashambulizi ya mara kwa mara hali iliyowalazimu wabunge kutunga
sheria za kusaidia kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Hofu ya usalama nchini Iraq imeendelea kuchochewa na uhasama kati kati
ya watu wa jamii za Washia na Wasunni na mgogoro wa kisiasa katika nchi
jirani ya Syria.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP watu zaidi ya 3000 wameuawa katika ghasia za nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka 2013
Post a Comment