
Miss
Tanzania 2012, Brigitte Alfred (kulia) akipokea hundi yenye thamani ya
shilingi Milioni 4.1 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Susan Omari jijini
Dar es Salaam jana. Fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la
wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya
Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Fedha hizo ni maalum kwaajili ya
kununulia mabati ya kuezekea bweni hilo. Kwa mujibu wa Brigitte zaidi
ya Shilingi milioni 60 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.
إرسال تعليق