Spika wa Bunge Zanzibar ataka baraza la wawakilishi kuwa na tahadhari katika kufanya maamuzi.


IMG_8852
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar.
Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho amesema Baraza la Wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuwajibika katika kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.
Hayo ameyasema  katika Baraza la wakilishi  wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura (CCM)  Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nje uzuiliwe kwani una wasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
Aidha asema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato.
Naye waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Muhamed Abuod Mohaamed amesema kuku wanao zalishwa na wananchi wa ndani ni tani 163 na nchi inahitaji tani 585 kwa kujitosheleza kimahitaji hivyo wazalishaji wa ndani bado uzalishaji wao mdogo

Post a Comment

أحدث أقدم