SYRIA:- MAGAIDI WATUMIA MWANYA WA MACHAFUKO KUBOMOA MISIKITI 1,400


Magaidi wabomoa Misikiti 1,400 nchini Syria
TAASISI ya Haki za Binadamu nchini Syria imeeleza kuwa, zaidi ya Misikiti 1,400 imebomolewa nchini humo tokea kuanza machafuko ya ndani yapata miaka miwili iliyopita. 

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo ya haki za binadamu nchini Syria inaeleza kuwa, tokea kuanza mashambulizi ya magaidi mwaka 2011 kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, zaidi ya misikiti 1450 na vituo kadhaa vya turathi za Kiisl
amu vimebomolewa kabisa. 

Taasisi hiyo imekosoa vikali uharibifu wa misikiti na vituo hivyo vya kidini vya Waislamu nchini Syria na kusisitiza kuwa, uharibifu huo hautawazuia kutekeleza ibada zao. 

Makundi ya kigaidi ambayo yanapata uungaji mkono wa kifedha, kisilaha na vyombo vya habari kutoka baadhi ya nchi za eneo  kama vile  Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na zile za kimataifa kama vile Marekani na Uingereza yameshadidisha mashambulizi dhidi ya Syria, nchi ambayo ni mhimili wa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

Post a Comment

أحدث أقدم