Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akizungumza na Waandishi wa Habari
wakati wa kuendesha droo ya pili kwa ajili ya kupata washindi katika
promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” ambapo washindi
saba wametangazwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya
Michezo ya kubahatisha Bw. Bakari Maggid na kushoto ni Meneja Bidhaa
wa Tigo Bw. Husni Seif.
Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif akibonyeza kitufe kuendesha droo hiyo kwa njia ya mtandao. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga.
Meneja
Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza kwa njia ya simu na
mmoja wa washindi kati ya saba wa “Miliki Biashara Yako” katika droo ya
pili ya promosheni hiyo ilyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif na kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Bakari Maggid wakishuhudia zoezi hilo.
Tigo
Tanzania leo imefanya droo yake ya pili katika promosheni yao kabambe
iitwayo “Miliki Biashara Yako” na kupata washindi wapya 7 wa wiki
iliyopita ambapo kila mmoja alijishindia Bajaji mpya yenye thamani ya
Tsh 6,700,000.
Washindi
hao ni Nicolus Maliyatabu Sanga (43) mkazi wa Dar, Julius Dilikwije
mkazi wa Same, Isabellah Edward Msemo (24)-Dsm, Eliasa Hamisi
Mbano(48)-Tabora, Charles Benedect Kato(41) – Kinyerezi Dsm, Evelyn
Elisalia Massawe (22) mwanafunzi mkazi wa Kimara Dsm na Khalidi Jafary
Gomani(27)-Dsm.
Akizungumza
katika mkutano na wanahabari waliohudhuria droo hiyo, Meneja Chapa wa
Tigo, Bw. William Mpinga aliwapongeza washindi hao na kutoa rai kwa
wateja wengine pia kushiriki katika promosheni hiyo.
“Kila
mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda
wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha
kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka
vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio
kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza
kuingia kwenye droo. Vile vile mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi
awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na
hayo, ili kuwapatia urahisi zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa
kuongeza salio pitia namna zote zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au
kwa vocha ya kawaida,” alisema Mpinga.
“Leo
Tigo imetimiza tena kwa hatua ingine jukumu letu tulionao katika
kuboresha na kugusa maisha ya Watanzania, kwa kuwapatia nafasi ya
kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya “Miliki Biashara
Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu wanapatiwa fursa ya
kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira, pamoja na kutoa
huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.”
Promosheni
hii inayalenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya
kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku
mteja atajishindia Bajaji moja.
“Tunaamini
kwamba promosheni hii itawapatia wateja wetu sababu nyingine
yakutabasamu. Wateja 60 watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji
mpya kabisa ambapo wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe.
Biashara ya Bajaji ni biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa
Bajaji anaweza kuingiza kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000
kwa siku, sawa na Tsh 900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa
mwaka,” alielezea Mpinga.
Bw.
Mpinga alisema kwamba kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari
Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na
bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja
kuchukua Bajaji yake na kuanzisha biashara yake mara moja,” alimalizia
Mpinga.
Wiki
iliyopita, Tigo ilifanya droo yake ya kwanza katika promosheni hii na
kupata washindi watatu ambao tayari wameshakabidhiwa Bajaji zao katika
hafla maalum iliyofanyika Soko Kuu, Kariakoo, wiki iliyopita.
Post a Comment