Tigo yapata washindi saba wapya katika droo ya pili ya “Miliki Biashara Yako”.


DSC_0871

Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kuendesha droo  ya pili kwa ajili ya kupata washindi  katika promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” ambapo washindi saba wametangazwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Bakari Maggid na kushoto ni  Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif.
DSC_0877
Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif akibonyeza kitufe kuendesha droo hiyo kwa njia ya mtandao. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga.
DSC_0881
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi kati ya saba wa “Miliki Biashara Yako” katika droo ya pili ya promosheni hiyo ilyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif na kulia ni  Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Bakari Maggid  wakishuhudia zoezi hilo.
Tigo Tanzania leo imefanya droo yake ya pili katika promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” na kupata washindi wapya 7 wa wiki iliyopita ambapo kila mmoja alijishindia Bajaji mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000.
Washindi hao ni Nicolus Maliyatabu Sanga (43) mkazi wa Dar, Julius Dilikwije  mkazi wa Same, Isabellah Edward Msemo (24)-Dsm, Eliasa Hamisi Mbano(48)-Tabora, Charles Benedect Kato(41) – Kinyerezi Dsm, Evelyn Elisalia Massawe (22) mwanafunzi mkazi wa Kimara Dsm na Khalidi Jafary Gomani(27)-Dsm.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari waliohudhuria droo hiyo, Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga aliwapongeza washindi hao na kutoa rai kwa wateja wengine pia kushiriki katika promosheni hiyo.
“Kila mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Vile vile mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na hayo, ili kuwapatia urahisi zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa kuongeza salio pitia namna zote zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au kwa vocha ya kawaida,” alisema Mpinga.
“Leo Tigo imetimiza tena kwa hatua ingine jukumu letu tulionao katika kuboresha na kugusa maisha ya Watanzania, kwa kuwapatia nafasi ya kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya “Miliki Biashara Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu wanapatiwa fursa ya kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira, pamoja na kutoa huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.” 
Promosheni hii inayalenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku mteja atajishindia Bajaji moja.
“Tunaamini kwamba promosheni hii itawapatia wateja wetu sababu nyingine yakutabasamu. Wateja 60 watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji mpya kabisa ambapo wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe. Biashara ya Bajaji ni biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa Bajaji anaweza kuingiza kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000 kwa siku, sawa na Tsh 900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa mwaka,” alielezea Mpinga.
Bw. Mpinga alisema kwamba kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja kuchukua Bajaji yake na kuanzisha biashara yake mara moja,” alimalizia Mpinga.
Wiki iliyopita, Tigo ilifanya droo yake ya kwanza katika promosheni hii na kupata washindi watatu ambao tayari wameshakabidhiwa Bajaji zao katika hafla maalum iliyofanyika Soko Kuu, Kariakoo, wiki iliyopita.

Post a Comment

أحدث أقدم