Wasanii
wa filamu nchini Jacob Stephen aka JB,Steve Nyerere na Bibi Kiroboto
wameingia mkataba mnono wa matangazo na kampuni ya Airtel utakaudumu kwa
muda wa mwaka mmoja.
Akiongea, Steve Nyerere amesema wameanza na mkataba wa
mwaka mmoja ambapo watafanya matangazo ya kampuni hiyo kuanzia kwenye
mabango ya barabarani, redioni na kwenye runinga.
Hata hivyo Steve hajaweka wazi kiwango alicholipwa kutokana na
mkataba huo wa kufanya matangazo ya Airtel Yatosha. Tayari barabarani
kuonekana mabango yenye sura za wasanii hao.
إرسال تعليق