Kampuni ya Apple
imetangaza programu ya kuuza USB power adaptors dunia nzima kwa punguzo
la nusu ya bei ya kawaida ili kukabiliana na charger feki
zinazofahamika zaidi kama ‘mchina’ hapa Tanzania.
Uamuzi huo wa Apple unafuatia ripoti iliyoonesha kuwepo kwa
charger nyingi feki zisizokidhi ubora na usalama wa mteja, kwa mujibu
wa taarifa ya Daily Mail.
Mfano mmoja wapo wa athari zitokanazo na charger feki ni lile la
msichana wa China Ma Ailun (23) aliyefariki mwezi uliopita kwa kupigwa
shoti wakati anaongea na simu ya iPhone iliyokuwa inachajiwa. Iligundulika kuwa charger aliyokuwa akitumia msichana huyo ilikuwa ni feki.

Kampuni hiyo imesema katika kipindi cha ofa charger hizo ‘USB power
adaptors’ zitapatikana kwa $10 ( 16,000 Tsh) kutoka bei ya kawaida
inayofikia $23 (37,000 Tsh).
Charger hizo original za bei ya ofa zitaanza kupatikana kuanzia
August 16 hadi October 18, na mteja yeyote atakayehitaji kununua
atahitajika kuonesha serial number ya iPhone, iPad au iPod na kukabidhi
charger yake (feki) ili apatiwe mpya.

Kama wewe ni mmoja kati ya walioshtushwa na lile tukio la msichana
aliyefariki akiwa anaongea na simu ya iPhone wakati anai charge, habari
hii itakuwa inakuhusu hivyo chukua hatua

إرسال تعليق