AJALI YA GARI LA TANESCO IMETOKEA USIKU HUU KWA SADALA MOSHI...

Toyota Corola lililosababisha ajali hii
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 Gari la shirika la umeme Tanzania (Tanesco) imepinduka usiku huu baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corola katika eneo la Kwa Sadala barabara ya Moshi/Arusha. 
 Kwa mujubu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari la Tanesco lilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea mjini Moshi. 
 Amesema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa zilizokuwa zikielekea Arusha ndipo akakutana na Loli hilo kabla ya kurudi  upande wake.
Ndipo gari magari hayo yakagongana na kisha gari la Tanesco kupinduka. Shuhuda  amesema majerhi wa ajali hiyo walikimbizwa hosptali ya KCMC huku dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusiko julikana. 

Askari wa usalama barabarani na gari la tanesco lililopinduka
Wadau eneo la  tukio

Post a Comment

Previous Post Next Post