Lydia Churi akiwauliza maswali mbalimbali wanafunzi kabla ya kuwapa bango hilo lenye picha za viongozi.Miongoni
mwa kazi za Idara hiyo ya Habari ya Serikali ni pamoja na kupiga picha
za viongozi na shughuli mbalimbali za serikali za kitaifa na
kuzihifadhi, kutoa nafasi ya kumbi za Mikotano baina ya watu mbalimbali
na Wanahabari.
--
IDARA
ya Habari MAELEZO ni Moja ya Taasisi za Serikali zilizo chini ya Wizara
ya Habari, vijana Utamaduni na Michezo ambayo ndio Idara yenye jukumu
la kusimamia na kuratibu shughuli zote za habari za Serikali na Taasisi
Zake.
MAELEZO
ikiwa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Idara ya habari inakusanya na
kusambaza habari zinazohusu utekelezaji wa Shughuli za seikali na
Maendeleo ya wananchi.
Pia ni Idara ambayo inahakikisha kuwa kunamawasiliano kati ya Serikali na wananchi.
Pichani Juu Afisa Habari Mwandamizi
kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Lydya Churi akitoa bango lililo na picha za
viongozi wa Serikali na Baraza la Mawaziri kwa wananchi wa Dodoma waliotembelea
banda la Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo lililopo katika Maonesho ya
Wakulima Nane Nane Nzuguni mkoani Dodoma jana.
إرسال تعليق