Mbunge Kigola |
Jesca Msambatavangu mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa( wa saba kutoka kushoto waliokaa) aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mpango wa kusomesha sekondari wanafunzi wasio wanaotoka familia zisizo na uwezo ujulikanao kama Mufindi Scholarship Program (MSP),akiwa na viongozi mbali mbali wa mradi huo ,wakuu wa shule za sekondari na 18 wilaya ya Mufindi, wanafunzi waliochaguliwa kusaidia kusomeshwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrad Kigola( wa tatu kulia waliokaa)
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akisalimiana na baba mzazi wa George Kavenuke Kulia
Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrad
Kigola amewataka wakuu wa shule na walimu katika wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa wasikubali kufundisha wanafunzi wanaosomea chini
ya ardhi . |
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana
katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi wakati wa hafla
ya uzinduzi wa mpango huo kuwasomesha watoto 81 elimu ya sekondari
unaojulikana kana Mufindi Scholarship Program (MSP)ulioanzishwa na
mashirika yasiyo ya kiserikali ya Muyodeso na Shalom Center .
|
Pamoja
na mbunge huyo kupongeza jitihada za mashirika hayo kwa kusaidia
elimu watoto hao wanaotoka familia masikini ila bado alisema kuwa
kutokana na wilaya ya Mufindi kuongoza kwa kilimo cha miti na kuwa na
msitu mkubwa wa Taifa msitu wa Sao Hill kamwe asingependa kuona
walimu wanaendelea kulia na uhaba wa madawati na hivyo kuwataka
walimu kususa kufundisha madarasa ambayo wanafunzi hawana madawati
ya kukalia.
|
"
Nawaombeni walimu kuanzia sasa msikubali kufundisha wanafunzi
wanaokaa chini ....nawaomba kila mkuu wa shule kutoa ripoti ya hali
halisi ya madawati katika shule yake kwa afisa elimu wa wilaya ili
kuwezesha kila shule kuwa na madawati "
|
Alisema
wilaya ya Mufindi ina utajiri mkubwa wa miti hivyo haipendezi kuona
wanafunzi wanakosa madawati ya kukalia na wanasomea ardhini .
|
Kwani alisema kwa upande wake
kama mbunge ameanza kulitafutia ufumbuzi suala hilo na amepata kutoa
msaada wa madawati katika shule mbali mbali za jimbo lake na kuwa
jitihada kama hizo pia zimefanywa na mbunge mwenzake wa jimbo la
Mufindi kaskazini .
|
Akielezea
kuhusu msaada wa mashirika hayo mawili yasiyo ya kiserikali ya Shalom
Center na Muyodeso ambayo yamejitolea kuwasaidia elimu ya
sekondari watoto 81 katika wilaya ya Mufindi alisema jitihada
hizo zinapaswa kuungwa mkono na serikali kwa kusaidia fedha zaidi
asasi hizo ili kuendelea kutoa msaada kwa watoto hao.
mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya mpango huo George Kavenuke alisema mpango
huo umelenga kuwasaidia watoto wa wilaya ya Mufindi ambao
wanauwezo mkubwa darasani ila wanashindwa kuendelea na masoni
kutokana na kutoka katika familia masikini . |
Kavenuke
alisema kuwa mradi huu unatekelezwa na Mashirika mawili ambayo ni
Muyodeso na Shalom centre for street children ambapo Shalom atakuwa
Shirika Kiongozi (lead Organization) na Muyodeso ikiwa ni asasi shiriki
katika mpango huo.
|
Alisema
kuwa katika kutekeleza maradi huo mashirika hayo yamelenga
kuwasaidia vijana 420 ambapo kiasi cha Tsh milioni 88,200,000
zinahitajika kwa hadi mwaka mwaka 2015 kwa ajili ya kuwalipia ada na
michango mbalimbali ya shule kutoka kidato cha tatu hadi cha sita
|
"Mradi
unalenga pia kuwahamasisha wadau wengine kuona umuhimu wa kutoa
misaada na huduma kwa vijana watokao katika familia masikini katika
shule za Kata na ambao uwezo wao wa kufaulu ni wa kuanzia daraja la
kwanza hadi la tatu..Kwa Mwaka huu 2013, tunatarajia kuwahudumia vijana
81 ambao wamefaulu ambapo jumla ya shilingi 17,010,000 zinahitajika ili
kuweza kuweza kugharamia ada, michango, vitabu na sare za shule"
|
Hata hivyo alisema kuwa uwezo
wa Mashirika hayo ni kuwalipia ada na michango mbalimbali ya kawaida na
mithihani. hivyo bado wanaomba jamii kujitokeza kusaidia zaidi vijana
hao kupitia mpango huo
|
Akielezea
utaratibu uliotumika kuwapata wanafunzi hao watakaoanza kunufaika na
mpango huo alisema mbali ya kuwashirikisha wakuu wa shule na
wadau wa elimu ila bado ilitungwa mitihani ya Masomo saba, kufanywa,
kusahihisha ambapo jumla ya vijana zaidi ya 100 walioteuliwa
kutoka shule zaidi ya 17 walifanya mtihani huo ila vijana hao 81
ndio waliopata ufaulu mzuri zaidi
|
إرسال تعليق