Miss Karun afanya makamuzi ya mwisho nnje ya Camp Mulla, Aweka wazi mipango yake nje ya kundi hilo


Msanii wa muziki ambaye amekuwa akifanya muziki wake na kundi la Camp Mulla, Miss Karun ametokea kwenye headlines baada ya kufanya poa katika moja ya maonyesho yake ya mwisho kabisa, Live at The Elephants jijini Nairobi, kabla ya kupaa kuelekea huko Marekani kwa ajili ya masomo.
      
 Miss Karun, ametangaza pia kuwaacha wapenzi wa muziki wake na albam mpya ambayo itatoka rasmi tarehe 16 mwezi huu, ambapo kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina Photoghraph.
Taio Tripper
Msanii huyu katika onyesho lake hili pia alipewa shavu juu ua jukwaa na msanii Taio Tripper ambaye na yeye kwa sasa anafanya kazi zake binafsi nje ya kundi la Camp Mulla, ambapo pia bendi kali ya muziki, Just a Band walikuwepo kufanya yap kwenye onyesho hilo.

Post a Comment

أحدث أقدم