Mzee
Zahir Ally Zoro, Msanii mkongwe wa muziki hapa Bongo ameamua kuwaomba
msamaha wanawake wote ambao amekwishakuwa nao katika maisha yake, na
wengine kuwapa ahadi kubwa kubwa ikiwepo kuwaoa, ambazo mwisho wa siku
hazikutimia.
Hii ni kupitia ngoma mpya ya Mzee huyu ambayo
inakwenda kwa jina Forgive Me, ambayo imefanyika chini ya producer
Lamar, kazi ambayo tayari imekamilika na mchakato wa kuisambaza upo
mbioni kuanza.

Mzee Zorro amesema wimbo huu unazungumzia
historia ya ukweli ya maisha yake ambapo amekiri kuwa amekwishakuwa
katika mahusiano mbalimbali ambayo mwisho wa siku hayakuwahi kufika
mahali.

Kaa tayari kwa kazi hii ambayo ina ujumbe mzito kwa maisha yao hivi karibuni, ikiwa katika miondoko ya Soul.
إرسال تعليق