SIKU moja baada ya Rais Robert Mugabe na Zanu PF
kutangazwa kushinda Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe, baadhi ya wafuasi wa
upinzani kutoka chama cha MDC wanasema wameshambuliwa na wenzao wa ZANU
PF.
Baadhi ya dola za Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza,
zimetilia shaka iwapo uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi. Madai hayo
yanakuja siku moja baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika
Jumatano kutolewa na kumpa ushindi rais Robert Mugabe. Chama chake
Zanu-PF kilipata thuluthi tatu ya viti vya bunge.
Watu 11 mjini Harare na wengine 20 kutoka mkoa wa Mashonaland,
wanasema kuwa walishambuliwa na wafuasi wa Zanu-PF wanaojulikana sana
baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Chama cha MDC kimesemna
uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya wizi wa kura. Kiongozi wake Morgan
Tsvangirai, ameahidi kuchukua hatua za kisheria kupinga matokeo ya
uchaguzi.
Pia alisema kuwa chama chake cha MDC, hakitashirikiana na kile cha
Mugabe na kuwa kitasusia kushikilia nafasi zozote katika taasisi za
serikali. Vyama hivyo viwili, vimekuwa wanachama wa serikali ya Muungano
tangu mwaka 2009, baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2008
kusababisha ghasia.
Watu 11 waliodai kushambuliwa katika mtaa mmoja mjini Harare waliomba
hifadhi katika makao makuu ya chama cha MDC mnamo Jumapili, kwa mujibu
wa mwandishi wa BBC Brian Hungwe. Wanadai kuwa walishambuliwa na wafuasi
wa Zanu-PF waliokuwa wanakwenda nyumba hadi nyumba wakiwaamuru wafuasi
wa MDC kufunga virago vyao na kuondoka.
Kiongozi wa chama cha MDC, Morgan Tsvangirai alisema uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya wizi.
Msemaji wa MDC, Douglas Mwonzora, alisema kuwa mashambulizi hayo yalipangwa. Lakini msemaji wa chama cha Zanu PF, Psychology Maziwisa, alikanusha madai kuwa wafuasi wa chama walikuwa wanawashambulia wapinzani wao.
Msemaji wa MDC, Douglas Mwonzora, alisema kuwa mashambulizi hayo yalipangwa. Lakini msemaji wa chama cha Zanu PF, Psychology Maziwisa, alikanusha madai kuwa wafuasi wa chama walikuwa wanawashambulia wapinzani wao.
MDC kinaonya kuwa hakitaweza kuwadhibiti wafuasi wake ikiwa madai ya
wao kushambuliwa yataendelea. Chama hicho kimeomba muungano wa nchi za
Kusini mwa Afrika, Sadc, kuingilia kati na kuzuia hali kuzorota zaidi
kiasi cha kutoweza jkudhibitiwa. Baadhi ya wakuu wa chama cha MDC,
wametoa wito kwa wafuasi wao kutoitii serikali na kutenga chama cha
Zanu-PF.
-BBC
-BBC

إرسال تعليق