Mrembo
na mwanamitindo Jokate Mwegelo anayejulikana pia kama Kidoti ameamua
kuvunja ukimya kwa kutoa maelezo juu ya tetesi zilizoenea mitaani kuwa
kuna uwezekano mrembo huyo kuwa (au wamewahi kuwa ) na uhusiano wa
kimapenzi na producer Luciano Gadie Tsere aka Lucci.
Haya yote ni matokeo ya video ya wimbo wa wawili hao ‘KAKA DADA’
iliyotoka hivi karibuni na kuonekana kuwashtua baadhi ya watu kutokana
na jinsi walivyoonekana kuwa na ukaribu wa ‘zaidi’ ya kuigiza kwenye
video,na kufanya watu wahisi Jokate na Lucci ni wapenzi.
Kupitia Instagram Jokate ameandika:
“Okay leo nimeamua kupitia page yangu ya Instagram ku-address the
following pressing matters kwenye ulimwengu wa majungu. 1. Luciano
Gadie Tsere is NOT my LOVER and noooo hatumegani kisela. Na hata kama it
were true inakuhusu nini. Sioni ishu. Kwenye Sanaa kuna kitu kinaitwa
kuweka uhalisia. And that’s what we did na KAKA DADA. I respect Lucci.
Ni kaka yangu na tunafanya kazi nyingi sana zinakuja. Kuna watu
wanefungua mpaka BBM group to discuss me and Lucci and this so called
affair. Jamani kuliko maneno tufanyeni Kazi kuendeleza nchi yetu 2.
Sijifanyi mtakatifu. Ila najitahidi kufanya matendo yanayompendeza
Mungu. Na kwasababu kama binadamu sina ukamilifu basi only God can
really judge me cause ndio anajua moyo wangu kuliko binadamu yoyote
yule. Ila I’m a pretty good girl to be honest. Najaribu. Kwa nyinyi
walimwengu don’t be fooled by my PRETTY BABY FACE I know what I want, am
fierce and I don’t take trying to tarnish my image easily. So kindly
don’t mess with KIDOTI. Msione mtu mkimya mkajua ndio wa kumuonea. Still
waters run deep 3. Yes there’s some guy I’m checking out. Like any
other female I deserve love cause I got so much love to give hey. So
whoever it is tafadhali tusiharibiane kwa maneno maneno. Have a blessed
evening!!!..”
Hivi karibuni, naye Lucci alilizungumzia suala hilo.
Kama hujabahatika kuiona video ya ‘Kaka Dada’ iliyofanyika nchini Kenya na kampuni ya Ogopa itazame hapo chini
Post a Comment