Lulu na Dr. Cheni ni ‘Baba na Mwana’, Lulu amwandikia ujumbe mzuri

lulu n cheni
Star wa filamu mpya ya ‘foolish age’ Elizabeth Michael a.k.a Lulu amempa cheo cha ‘baba’ msanii mwenzake wa filamu nchini Dr. Cheni na kumshukuru kwa mapenzi na sapoti aliyoionesha kwake.
Lulu ameweka picha Instagram akiwa amesimama kwa pozi na mwenye furaha mbele ya Dr. Cheni na kuandika, “Tnx 4 ur LOVE & SUPPORT baba!!!”
Dr. Cheni kwa Lulu anaweza kuwa baba hasa katika tasnia ya filamu kwa kuanza kuangalia wakati Lulu anaanza kuigiza akiwa na umri mdogo sana, Dr.Cheni ni moja kati ya watu waliokuwa wanamwagilia mti wa kipaji chake na sasa hivi unatoa matunda mema.
Lakini pia sifa ya baba inategemea kile alichofanyiwa na Dr. Cheni, wengi tulishuhudia wakati wa matatizo yaliyomkuta Lulu jinsi ambavyo Dr. Cheni alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha anamsapoti na kumfariji kiasi ambacho baadhi ya watu walianza kuweka alama za ‘???’ kichwani kuhusu uhusiano wao.

Post a Comment

Previous Post Next Post