Mwandishi wa habari za michezo Tanzania( Bin Zubeiry) atishiwa

Picture: Mahmoud ZubeiryBin Zubeiry

Mwandishi na mchambuzi wa habari za michezo nchini Tanzania, Mahmoud Zubeiry ameandika waraka katika blogu yake ya BongoStaz akizungumzia kuhusu vitisho vilivyoelekezwa kwake kutokana na msimamo wake wa jinsi anavyotafsiri hali ya michezo.

Mathalan, katika chapisho hilo Mahmoud anasema, “Tangu mwaka 1996 hadi leo, ni orodha ndefu ya matukio niliyowahi kukutana nayo yenye kumaanisha ugumu na kuhatarisha maisha yangu. Kuvamiwa na kundi la wapenzi wa klabu kubwa za Simba na Yanga na kutaka kupigwa, mara nyingi tu, kisa tu umeandika habari ambayo haijawapendezea, pasipo kuzingatia ukweli wa mambo.

Kutiwa kashikashi na mikwara na viongozi wa klabu kubwa, makocha au wachezaji kisa umeandika habari ambayo hawajaipenda. Kujengewa chuki na kufitinishwa, kusingizwa kashfa mbaya, watu kuingilia hadi maisha yako binafsi, zote ni changamoto ambazo nimekutana nazo katika tasniya hii ya Habari.”

Ametolea mfano wa kisa kimoja kilichomtokea mwezi Desemba akiwa kazini huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo anasema alitekwa, akapigwa na kuporwa fedha wakati akitoka kwenye kambi ya klabu ya Azam akirejea hotelini.

Lakini pamoja na yote hayo, Mahmoud hajaacha kuwapa matumaini wasomaji wake kwani amesema: "Nataka niwahakikishie wapendwa wasomaji wangu maelfu waliojenga imani na mimi kwamba, nitaendelea kuandika ukweli bila woga. Nitaendelea kutenda haki katika kazi. Nitajitahidi, kutoegemea upande wowote, bali kuzingatia misingi ya haki katika Uandishi bila kumuonea mtu." Bofya hapa kusoma waraka huo wenye kichwa cha habari, “UMEFIKA WAKATI YANGA WABADILIKE...” 

Post a Comment

أحدث أقدم