Polisi Dar yaanza kulinda benki zote za mkoa huo

 
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kuwa kuanzia leo, Jumatatu Septemba 30, 2013 benki zote zilizopo jijini Dar es Salaam zitalindwa na jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishina wa Polisi, Suleiman Kova alisema kuwa hatua hiyo imetokana na vitendo vya kihalifu vinavyoendelea kushamiri katika benki  na hivyo kwa kuwa ni kamishina wa polisi wa kanda hiyo, ametoa agizo kwa makamanda wote kujipanga upya dhidi ya matukio ya kihalifu: “Kuanzia Septemba 30, 2013, benki zote za jijini Dar es Salaam zitalindwa na Jeshi la Polisi wenye sare na silaha kwa kusaidiana na walinzi wa benki hizo,” alisema.

Aliongezea kuwa matukio yote yaliyojitokeza inaonekana ni watu walewale kwani mbinu wanazozitumia zinafanana, hivyo anaamini kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wa benki wanashirikiana na majambazi kwa kutoa taarifa na siri za benki.

Aliwashauri wamiliki wa benki kuweka CCTV ili kuweza kufuatilia mwenendo mzima wa benki, kukagua watu wote kwa kutumia vifaa maaulumu ili kuweza kubaini vitu vyenye asili ya chuma kabla ya kuingia ndani ya benki. --- Tanzan

Post a Comment

Previous Post Next Post