Na.Mo Blog Team
Mcheza
tenisi wa kike namba moja duniani, Serena Williams, amefikia rekodi ya
Roger Federer ya kushinda mashindano mengi kwa wanaume baada ya
kumshinda mchezaji namba mbili duniani, Victoria Azarenka, katika mchezo
uliochukua muda mrefu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 kwenye
mashindano ya wazi ya US.
Williams
allifikia rekodi hiyo kushinda vikombe vikubwa 17 kwa ushindi wa seti
7-5 6-7 (6-8) 6-1 katioka mchezo uliodumu kwa masaa mawili na dakika 45
uliochezwa Jumapili.
“Yeah, hii safi sana,” alisema Williams baada ya kuifikia rekodi ya Mswisi Federer.
Willimas
mwenye umri wa miaka 3, pia amekuwa mwanamke mwenye umri mkubwa
kushinda mashindano ya wazi jijini New York, ikiwa ni siku 293 zaidi ya
umri wa Margaret Smith Court ambaye alishinda mwaka 1973.
Williams
amepata dola za Kimarekani milioni 3.6 pamoja na nyongeza ya dola za
Kimarekani milioni moja kwa kufanikisha matukio kabla ya mashindano
hayo.
Post a Comment