Johari aangukia kwenye penzi la Mcanada, aenda kujitambulisha ukweni

100_5722Muigizaji wa filamu nchini Blandina Chagula aka Johari yupo nchini Canada alikoenda kujitambulisha kwa ndugu wa mchumba wake pamoja na kupanga taratibu za harusi yao.
Akizungumza jana, Irene Uwoya ambaye ni rafiki wa karibu na Johari amesema kuna mzungu wa nchini Canada aliyetokea kumpenda Johari nakumtaka kwenda kumtambulisha kwao na kuweka mambo sawa.
“Akitambulishwa kitachofuata ni ndoa,kwa jinsi tulivyojadiliana watafanya ndoa mbili, moja hapa na nyingine Canada, ili na sisi tulio Dar es salaam tusheherekee ndoa yake kwasababu kama unavyojua ndugu zake ,marafiki na watanzania kwa ujumla wanahitaji kushuhudia ndoa yao,” alisema Irene.
“Juzi niliandika kauli ya kumtaka atulie akiwa Canada, sio kwamba Johari hajatulia ila unajua Johari ni mtu wangu wa karibu,kwahiyo nilikuwa namwambia abadilike asipeleke uswahili Canada sio kwa nia mbaya.”

Post a Comment

Previous Post Next Post